Pata taarifa kuu
MAREKANI-BIDEN-CORONA-AFYA-UCHUMI

Joe Biden atangaza kuunda Jopo la wataalam kuhusu Covid-19

Jopo hili la "wataalam mashuhuri" litateuliwa kuanzia Jumatatu na litatakiwa kuanzisha mpango wa utendaji kuanzia Januari 20, 2021, siku ya kuapishwa kwa rais mpya.

Joe Biden ametangaza kwamba ataanzisha kitengo cha kukabiliana na ugonjwa huo hatari kuanzia Jumatatu, Novemba 9, akiwaleta pamoja "wanasayansi mashuhuri na wataalam" kupambana na changamoto kuu inayoikabili sasa serikali ya Marekani.
Joe Biden ametangaza kwamba ataanzisha kitengo cha kukabiliana na ugonjwa huo hatari kuanzia Jumatatu, Novemba 9, akiwaleta pamoja "wanasayansi mashuhuri na wataalam" kupambana na changamoto kuu inayoikabili sasa serikali ya Marekani. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Joe Biden amekua akilitaja jopo hili kila mara katika hotuba yake: vita dhidi ya janga la Covid-19, ambalo limeua watu 237,000 nchini Marekani itakuwa kipaumbele chake cha kwanza. Kwa kufanya hivyo, Joe Biden ametangaza kwamba ataanzisha kitengo cha kukabiliana na ugonjwa huo hatari kuanzia Jumatatu, Novemba 9, akiwaleta pamoja "wanasayansi mashuhuri na wataalam" kupambana na changamoto kuu inayoikabili sasa serikali ya Marekani.

"Jumatatu, nitaanzisha nitateuwa jopo la wanasayansi na wataalam" kufanya kazi "juu ya mpango ambao utaanza kutumika mnamo Januari 20, 2021", siku ya kuapishwa kwangu, amesema rais mteule mbele ya umati wa wafuasi wake walikusanyika huko Wilmington, Delaware kusherehekea ushindi wake.

Katika wiki hii ya uchaguzi wa urais, Marekani imerekodi idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya Corona kutokana na mlipuko mpya wa janaga hilo kwa siku kadhaa. Marekani ilirekodi zaidi ya visa vipya 122,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona siku ya Jumamosi kwa muda wa saa 24, kulingana na takwimu za shirika la habari la AFP zilizotolewa saa mbili na nusu usiku kwa kutumia takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

Wakati huo huo, watu 991 wamefariki dunia kutokana na virusi hivyo nchini Marekani, nchi ambayo imerekodi vifo vingi duniani kutokana na ugonjwa huo. Kufikia Jumamosi nchi hii yenye nguvu duniani ilirekodi jumla ya vifo zaidi ya 237,000 tangu kuzuka kwa janga hilo, na visa milioni 9.8 vya maambukizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.