Pata taarifa kuu
MAREKANI-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa Merika 2020: Fuatialia ushindi wa kihistoria wa Joe Biden

Mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden amechaguliwa kuwa rais wa 46 wa Marekani mnamo Novemba 7, 2020, baada ya kampeni isiyo kuwa ya kawaida na mchakato wa uchaguzi uliyodumu siku nne kabla ya kujua matokeo ya mwisho.

Joe Biden katika kampeni huko Philadelphia, Juni 2020.
Joe Biden katika kampeni huko Philadelphia, Juni 2020. AP Photo/Matt Slocum
Matangazo ya kibiashara

Zoezi la kukabidhiwa madaraka kati ya Donald Trump na mrithi wake litafanyika Januari 20, 2021.

► Mgombea wa chama cha Democratic Joe Biden alishinda uchaguzi wa urais wa Marekani, baada ya kushinda jimbo muhimu la Pennsylvania kwa kupata wajumbe maalumu 20. Kulingana na vyombo vya habari, alizidisha idadi ya 270 inayohitajika kutangazwa mshindi, na kupata kati ya 273 na 284, dhidi ya 214 aliopata Donald Trump.

► Hata hivyo zoezi la uhesabuji wa kura linaendelea, kwani majimbo ya Georgia, Arizona, Nevada na North Carolina bado hayajatangaza matokeo yao ya mwisho. Georgia ilitangaza kuwa itarejea kuhesabu upya kura zake.

► Muda mfupi baadaye, Rais anayemaliza muda wake Donald Trump alimshtumu Joe Biden kwa "kukimbilia kujitangaza" mshindi, katika taarifa, na kuongeza kuwa timu yake itatetea kesi yake mahakamani. Alikuwa tayari alisema atagfungua kesi kwenye Mahakama Kuu.

► Kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter, Joe Biden alielezea furaha yake kuchaguliwa kuwa rais wa 46 wa Marekani: "Nitakuwa rais wa Wamarekani wote". Jioni ya Novemba 7, alitoa hotuba yake ya ushindi hko Chase Cenyer katika mji wake wa Wilmington.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.