Pata taarifa kuu
MAREKANI-MAJANGA ASILI-USALAMA

Marekani: San Francisco yakumbwa na kisa cha moto ambao haujawahi kutokea

Moto mkubwa umeharibu miji mitano katika jimbo la Oregon nchini Marekani na unaendelea kusambaa katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo na kuzua hali ya wasiwasi.

Moto huo ulianzia katika misitu ya jimbo hilo na kusamlbaa kwa haraka kutokana na upepo mkali katika jimbo hilo ambalo ukubwa wake ni mara mbili zaidi ya New York.
Moto huo ulianzia katika misitu ya jimbo hilo na kusamlbaa kwa haraka kutokana na upepo mkali katika jimbo hilo ambalo ukubwa wake ni mara mbili zaidi ya New York. Philip Pacheco/Getty Images/AFP
Matangazo ya kibiashara

Moto huo wa kihistoria unaendelea kuteketeza misitu katika jimbo la Oregon, Washington na California. Jiji la San Francisco lilijikuta limetumbukia kwenye giza Jumatano kutokana na moshi wa moto wa nyika. Hali inayowasumbua wakazi wa mji huo.

Moto huo ambao umekumba pwani nzima ya magharibi mwa Marekani kwa wiki kadhaa, kutoka mpaka wa Canada hadi mpaka wa Mexico, haujawahi kutokea kabisa na tayari watu nane wamepoteza maisha na eneo lenye kilomita mraba 10,000 limeteketea kwa moto huko California pekee.

Ripoti zinasema kuwa mbali na uharibifu wa majengo na vitu vingine, vifo vya watu vimeripotiwa na kuna wasiwasi kuwa hali huenda ikawa mbaya zaidi na kuleta madhara makubwa.

Moto huo ulianzia katika misitu ya jimbo hilo na kusamlbaa kwa haraka kutokana na upepo mkali katika jimbo hilo ambalo ukubwa wake ni mara mbili zaidi ya New York.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.