Pata taarifa kuu
MAREKANI-IRAQ-TRUMP-USALAMA

Idadi ya wanajeshi wa Marekani kupunguzwa Iraq

Rais wa Marekani Donald Trump anatarajia leo Jumatano kutangaza hatua mpya ya kupunguza wanajeshi wa nchi hiyo walioko nchini Iraq, kulingana na mwakilishi wa utawala wa Marekani.

Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa hotuba yake baada ya kuapishwa kama mgombea wa urais Agosti 27, 2020 huko Ikulu ya White House.
Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa hotuba yake baada ya kuapishwa kama mgombea wa urais Agosti 27, 2020 huko Ikulu ya White House. CHIP SOMODEVILLA / GETTY IMAGES NORTH AMERICA / Getty Images via
Matangazo ya kibiashara

Tangazo lingine kuhusu kupunguzwa kwa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan litatolewa katika siku zijazo, chanzo hicho kimeongeza.

Hatua hiyo inakuja wakati Donald Trump anakabiliwa na utata juu ya matamshi ya dharau ambayo inasemekana alitoa juu ya wanajeshi wa Marekani waliouawa katika vita.

Tangazo hilo linaweza kuwa na lengo la kuwashawishi wapiga kura kwamba Donald Trump anatarajia kutekeleza ahadi yake ya kuhitimisha kile alichoelezea kama "vita visivyo na mwisho."

Merika ina wanajeshi karibu 5,200 waliopelekwa nchini Iraq kupigana dhidi ya kundi la Islamic State.Karibu wanajeshi 8,600 wa Marekani walipelekwa nchini Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.