Pata taarifa kuu
MAREKANI-WHO-CORONA-AFYA

Donald Trump atishia kusitisha mchango wa Marekani kwa WHO ndani ya siku 30

Rais wa Marekani, Donald Trump ametangaza kwamba usitishwaji wa mchango wa Marekani kwa Shirika la Afya Duniani, WHO, utaanza kutekelezwa mara moja ndani ya siku thelathini, ikiwa shirika hilo halitafanya "maboresho" makubwa.

Rais wa Marekani Donald Trump , ambaye anakabiliwa na uchaguzi mkuu mwaka huu ambaye amekosolewa jinsi anavyotatua ugonjwa huo nchini Marekani , amelaumu China kwa kujaribu kuziba mlipuko huo na kuilaumu WHO kwa kushindwa kuiwajibisha China.
Rais wa Marekani Donald Trump , ambaye anakabiliwa na uchaguzi mkuu mwaka huu ambaye amekosolewa jinsi anavyotatua ugonjwa huo nchini Marekani , amelaumu China kwa kujaribu kuziba mlipuko huo na kuilaumu WHO kwa kushindwa kuiwajibisha China. MANDEL NGAN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Marekani imelishutumu Shirika la Afya Duniani kwa kuruhusu ugonjwa wa Covid -19 kushindwa kudhibitika na kupuuzia hatari ya ugonjwa huo, ambao umesababisha vifo vya maelfu ya watu duniani.

Mlipuko wa Corona tayari umewauwa zaidi ya watu 316,000 ulimwenguni, na Merika ndio nchi iliyoathiriwa zaidi na vifo vya zaidi ya watu 90,000 na karibu watu milioni 1.5 wameambukizwa virusi vya Corona.

Rais Trump ambaye ameendelea kukosoa Shirika hilo la kimataifa kwa usimamizi wake dhidi ya janga la Covid-19, ametoa mwezi mmoja kwa WHO kupata matokeo muhimu.

"Iwapo WHO haitafanya maboresho makubwa ndani ya siku 30, nitabadilisha uamuzi wa awali wa kusitisha kwa muda mchango wa fedha wa Marekani kwa shirika hilo na kuchukuwa hatu muhimu na kusitisha uanachama wetu kwa Shirika la Afya Duniani" , Bw. trump ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Rais wa Marekani Donald Trump, ambaye anakabiliwa na uchaguzi mkuu mwaka huu ambaye amekosolewa jinsi anavyotatua ugonjwa huo nchini Marekani , amelaumu China kwa kujaribu kuziba mlipuko huo na kuilaumu WHO kwa kushindwa kuiwajibisha China.

Wakati huo huo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema tathmini huru ya jinsi janga la virusi vya Corona linavyoshughulikiwa itaanzishwa haraka iwezekanavyo na China imeunga mkono hatua hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.