Pata taarifa kuu

Rais wa Marekani alishukia shirika la Afya Duniani WHO na kulitishia kulikatia fedha

Rais wa Marekani Trump ametishia kulikatia fedha shirika la afya Duniani WHO kwa sababu amesema shirika hilo halikutilia maanani kwa namna ilivyopasa hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.

Donald Trump ameonywa mara mbili kuhusu hatari ya ugonjwa Covid-19.
Donald Trump ameonywa mara mbili kuhusu hatari ya ugonjwa Covid-19. REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati nchi hiyo imerekodi vifo vingi vya ugonjwa wa corona kwa siku huku watu 1,736 wakifariki siku ya Jumanne.

Watu ambao wamefariki dunia kwa ugonjwa hatari wa Covid-19 wamefikia 12,722 kulingana na takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins.

Trump amelilaumu shirika hilo kwa kuegemea zaidi upande wa China. Rais huyo wa Marekani amedai kwamba asasi hiyo ya kimataifa ilishirikiana na China katika miezi kadhaa iliyopita kupuuza hatari ya maambukizi ya virusi vya corona.

Visa 398,000 vya maambukizi vilivyothibitishwa vinaripotiwa nchini Marekani, hii ikiwa ndio idadi kubwa zaidi duniani.

Hata hivyo katika mkutano na waandishi habari Jumanne wiki hii, rais Trump alisema kwamba huenda Marekani ikaripoti visa vichache zaidi ya ilivyotabiriwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.