Pata taarifa kuu
MAREKANI-TRUMP-HAKI

Trump ashtakiwa juu ya ujumbe wa Twitter

Wakili wa mwigizaji wa filamu za ngono Stormy Daniels anasema mteja wake amemshtaki Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu ujumbe wa Twitter anaodai ni wa kumharibia jina.

Stormy Daniels, mwigizaji nguli wa filamu nchini Marekani anaedai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump mwaka 2006.
Stormy Daniels, mwigizaji nguli wa filamu nchini Marekani anaedai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump mwaka 2006. AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakili wa Bi Daniel aliandika kwenye Twitter kwamba Bw Trump "anafahamu vyema kabisa yaliyotokea".

Hivi karibuni Stormy Daniels alifichua uhusiano wa kimapenzi uliokuepo kati yake na rais Donald Trump kabla hajaingia ikulu ya White House.

Bi Daniels anasema yeye na rais huyo walikuwa na uhusiano wa kimapenzi kuanzia 2006.

Bi Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, anasema alitishiwa na mwanamume mmoja katika maegesho ya magari mjini Las Vegas na kutakiwa kuacha kuendelea na madai yake kwamba aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Donald Trump.

Wakili wa Trump alidaiwa kumlipa mwigizaji wa filamu za ngono ili aweze kunyamaza.

Rais Donald trump alichapisha kwenye Twitter mchoro wa mwanamume mshukiwa na kisha kuandika "hii ni kazi ya utapeli kabisa".

Bi Daniels awali alimshtaki wakili wa Bw Trump, Michael Cohen, akitaka kuvunjwa kwa mkataba wa kutofichua siri kuhusu uhusiano huo, ambao anasema Bw Trump hakuutia saini.

Bw Cohen awali alikiri kwamba alimpa Bi Daniels Dola 130,000 zake mwenyewe, lakini alisema kwamba hakueleza ni kwa nini alitoa fedha hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.