Pata taarifa kuu
MAREKANI-DONALD TRUMP

Muigizaji wa filamu za ngono asema anatishiwa maisha na rais Trump

Muigizaji wa filamu za ngono Stormy Daniels anasema ametishiwa maisha yake katika jaribio la kumfanya akae kimya kuhusu uhusiano wake na rais wa Marekani Donald Trump, katika mahojiano ya kina na kituo kimoja cha televisheni.

Stormy Daniels, mwigizaji nguli wa filamu nchini Marekani anaedai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump mwaka 2006.
Stormy Daniels, mwigizaji nguli wa filamu nchini Marekani anaedai kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Rais wa sasa wa Marekani Donald Trump mwaka 2006. AFP
Matangazo ya kibiashara

Muigizaji huyo sasa anataka kutolewa kwenye makubaliano ya kukaa kimya ambayo alitia saini siku 11 kabla ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2016, uchaguzi ambao ulimuweka madarakani rais Trump, ambapo alilipwa kiasi cha dola za Marekani laki 1 na elfu 30, malipo yaliyibua maswali kuhusu mahali fedha hizo zilipatikana.

Daniels amemwambia wanahabari wa kituo cha CBS Anderson Cooper kuwa rais Trump hakumuomba kuufanya uhusiano wao kuwa siri lakini akasema alifuatwa na mtu alipokuwa mjini Las Vegas baada ya kukubali kuiuza habari yake kwa dola elfu 15 mwaka 2011.

“Nilikuwa kwenye eneo la kuegesaha magari, nikijiandaa kwenda kwenye mazoezi na mtoto wangu. Nikimchukua kutoka siti ya nyuma,” akieleza kwa kutumia lugha ya mafumbo.

“Mtu huyo alikuja na akaniambia ‘muache Trump. Sahau kuhusu habari.’ na baada ya hapo akageuka nyuma kumuangalia mwanangu na kusema ‘huyu ni mtoto mzuri. Itakuwa ni aibu kitu chochote kikimtokea mama yake,” alisema Daniels.

Mwanahabari huyo alimuuliza tena “ulichukulia kama kitisho cha moja kwa moja?” swali ambalo Daniels alijibu “Ndio.”

“Niliogopa, nakumbuka wakati nikienda darasa la mazoezi mikono yangu ilikuwa ikitetemeka, nilikuwa naogopa na hata ningeweza kumuangusha,” alisema kuigizaji huyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.