Pata taarifa kuu
SIASA-MAREKANI

Obama asema Bi.Clinton anatosha kuwa rais wa Marekani

Rais wa Marekani Barrack Obama kwa mara ya kwanza ameungana na Bi.Hillary Clinton katika kampeni ya kuomba kura kuelekea uchaguzi Mkuu mwezi Novemba mwaka huu.

Hillary Clinton na Barrack Obama wakiwa katika kampeni ya kisiasa katika jimbo la North Carolina
Hillary Clinton na Barrack Obama wakiwa katika kampeni ya kisiasa katika jimbo la North Carolina REUTERS/Brian Snyder
Matangazo ya kibiashara

Obama na Clinton wamekuwa katika jimbo la North Carolina, kukutana na wapiga kura kuwarai kukipigia kura chama cha Democratic.

Rais Obama amesema anaamini Clinton ndio mtu pekee anayeweza kumrithi kwa sababu ana uwezo wa kuwa rais wa nchi hiyo.

Aidha, ameongeza kuwa Bi.Clinton ana uzoefu mkubwa wa kufanya kazi baada ya kushiriki katika vikao mbalimbali vya maamuzi wakati alipohudumu kama Waziri wa Mambo ya nje.

Rais Barrack Obama na Bi.Hillary Clinton
Rais Barrack Obama na Bi.Hillary Clinton REUTERS/Jim Young

Clinton anatarajiwa kukumenyana na mpinzani wake Donald Trump kutoka chama cha Republican katika uchaguzi huo.

Akizungumza katika mkutano huo wa kisiasa, mgombea huyo amesema Trump ni mtu ambaye hana uwezo wa kuongoza nchi hiyo.

Wakati hayo yakijiri, Shirika la ujasusi la Marekani FBI limetangaza kuwa halitapendekeza kufunguliwa mashtaka dhidi ya Bi. Clinton kwa kutumia anwani yake ya kibinafsi kutuma na kupokea taarifa za siri za serikali.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo James Comey amesema pamoja na kwamba Bi .Clinton kutumia visivyo anwani yake ya kibinafsi, hilo halitoshi kufungiliwa mashtaka.

Uamuzi huu wa FBI unafunga uchunguzi uliokuwa unaendelea dhidi ya mgombea huyo kwa muda mrefu kwa matumizi mabaya ya anwani hiyo.

Mgombea wa Republican Donald Trump ameshtumu uamuzi huo na kusema FBI imeamua kumfunika Bi.Clinton na kuongeza kuwa hatua hiyo imehatarisha usalama wa Marekani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.