Pata taarifa kuu
SIASA

Hillary Clinton ahojiwa na FBI

Maafisa wa ujasusi nchini Marekani FBI wamemhoji mwanasiasa wa chama Democratic na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nje, Hillary Clinton kuhusu madai ya kutumia anwani yake binafsi ya barua pepe kufanya kazi za Wizara hiyo.

Waziri wa zamani wa Mambo ya nje na mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic Bi.Hillary Clinton
Waziri wa zamani wa Mambo ya nje na mgombea wa urais kupitia chama cha Democratic Bi.Hillary Clinton EUTERS/Rick Wilking
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya maswala ya Sheria na Haki nchini humo inamtuhumu Clinton kwa kwenda kinyume na maadili ya kazi na hivyo kutaka kuchunguzwa na kufunguliwa mashtaka ya kutumia anwani yake kutuma na kuhifadhi taarifa za siri.

Ripoti zinasema kuwa Bi Clinton ambaye anatarajiwa kuwania urais kupitia chama cha Democratic mwezi Novemba mwaka huu, alihojiwa kwa muda wa saa 3.

Clinton amekuwa akisema hakuwahi kutumia visivyo anwani yake wakati alipokuwa katika wadhifa huo na badala yake kusema wanapinzani wake wanampaka tope.

Msemaji wake, amesema mahojiano kati ya Clinton na maafisa hao wa FBI yalikuwa ya kirafiki na alijitolea kwenda kuhojiwa ili kusaidia kutoa mwangaza kuhusu tuhma dhidi yake.

Katika mahojiano hayo Clinton amesema alilazimika kufungua anwani nyingie akitumia simu yake ya mkononi ili kufaya kazi zake kwa urahisi lakini hakuwahi kuitumia kutuma taarifa za siri kama inavyodaiwa.

Wakosoaji wake hasa mpinzani wake Donald Trump kutoka chama cha Republican, wamekuwa wakisema hatua ya kutumia anwani yake binafsi ni kuonesha kuwa si mwaminifu katika kazi zake na hivyo hawezi kuaminiwa kuwa rais wa Marekani.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.