Pata taarifa kuu
CHINA-CORONA-AFYA

China yaendelea kukabiliana na kuenea kwa virusi vya Covid-19

China imetangaza Jumatano (Machi 4) kupungua kwa idadi ya kesi mpya za maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari unaofahamika kama Covid-19 kwa siku ya tatu mfululizo, huku vifo vipya 38 vikiripotiwa.

Mamlaka ya afya nchini China imesema leo Jumatano kwamba Jumanne wiki hii iligundua kesi mpya 119 za maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari unaofahamika kama Covid-19 na kuripoti vifo vipya 38 vilivyosababishwa na ugojnwa huo katika China Bara.
Mamlaka ya afya nchini China imesema leo Jumatano kwamba Jumanne wiki hii iligundua kesi mpya 119 za maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari unaofahamika kama Covid-19 na kuripoti vifo vipya 38 vilivyosababishwa na ugojnwa huo katika China Bara. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya vifo katika ngazi ya kitaifa sasa imefikia 2,981, tume ya kitaifa ya afya imesema, na zaidi ya jumla ya watu 80,200 wameambukizwa virusi hivyo nchini tangu ugonjwa huo kuzuka katika mji wa Wuhan mwezi Desemba mwaka jana.

Mamlaka ya afya nchini China imesema leo Jumatano kwamba Jumanne wiki hii iligundua kesi mpya 119 za maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari unaofahamika kama Covid-19 na kuripoti vifo vipya 38 vilivyosababishwa na ugojnwa huo katika China Bara.

Kwa mujibu wa shirika la utangazaji la REUTERS, kati ya vifo vipya, 37 vimeripotiwa katika mkoa wa Hubei, katikati mwa nchi, ambapo ugonjwa huo ulianzia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.