Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-AFYA-CORONA

Coronavirus: Kesi mpya 600 za maambukizi zathibitishwa Korea Kusini

Korea Kusini imetangaza kesi mpya 600 za maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Covid-19 nchini humo, na idadi hiyo inakamilisha watu 4,812 walioambulizwa virusi hivyo tangu ugojnwa huo ulizuka katika China Bara mwezi Desemba, mamlaka ya afya wamesema.

Wanajeshi wa Korea Kusini katika zoezi la kupambana na kuenea kwa virusi vya Covid-19 huko Daegu, Februari 29, 2020.
Wanajeshi wa Korea Kusini katika zoezi la kupambana na kuenea kwa virusi vya Covid-19 huko Daegu, Februari 29, 2020. Yonhap via REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake ya kila siku, Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (KCDC) pia kimethibitisha vifo vipya vitatu. Watu thelathini na nne wamefariki dunia nchini Korea Kusini kutokana na virusi hivyo, kituo hicho kimebaini katika taarifa, kwa mujibu wa shirika la Utangazaji la Reuters.

Kesi nyingi zimeripoitwa huko Daegu, mji unaopatikana Kusini-Mashariki mwa nchi ambapo kuna kundi la kidini ambalo haliitikii wito wa kujizuia au kujilinda na ugonjwa huo.

Mwanzilishi na kiongozi wa kundi hilo la kidini la Shincheonji, Lee Man-hee, ametaja mlipuko wa ugonjwa huo wa Covid-19 kama "janga" na akaomba msamaha kwa kuenea kwake, huku akikataa kufanya vipimo.

Maafisa wa afya Kusini mwa Korea walimlazimisha Lee Man-hee kufanya vipimo. Mwakilishi kutoka Mkoa wa Gyeonggi, ambaye hakutaka jina lake litajwe, amebaini kwamba kiongozi huyo wa kidini hakupatikana na dalili zozote za ugojnwa wa Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.