Pata taarifa kuu
KENYA-CHINA-AFYA-CORONA

Coronavirus: China Southern Airlines yatua Nairobi, raia waingiliwa na wasiwasi

Baada ya kusitisha safari zake za kwa wiki mbili ili kujaribu kuzuia kuenea kwa virusi vya Covid-19, shirika la ndege la China Southern Airlines limeanzisha tena safari zake kati ya China na Kenya.

Airbus A380, ndege ya shirika la ndege la China Southern Airlines Oktoba 14, 2011.
Airbus A380, ndege ya shirika la ndege la China Southern Airlines Oktoba 14, 2011. AFP/ PASCAL PAVANI
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano, ndege kutoka Guangzhou ilitua kwenye Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta. Uamuzi ambao umeibua mvutano mkubwa, wakati virusi vya Covd-19 vinaendelea kusambaa duniani kote.

Picha ya ndege hii imesambazwa kwenye mitandao ya kijamii nchini Kenya. Ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria 329. Wengi wao wakiwa ni raia wa China.

Kulingana na Wizara ya Afya ya Kenya na ubalozi wa China nchini Kenya, tahadhari zote zimechukuliwa. Na wamewataka wasafiri kujiweka karantini wenyewe. Hatua ambayo imezua wasiwasi mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.