Pata taarifa kuu
MAREKANI-KOREA KUSINI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Marekani na Korea Kusini waahirisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi

Marekani na Korea Kusini zimeahirisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi leo Alhamisi kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid-19 katika nchi hii ya Asia ambapo idadi ya kesi mpya za maambukizi imeongezeka kwa robo, na kufikia 1.595 watu walioambukizwa virusi hivyo.

Wafanyakazi wa afya wakisubiri gari ya wagonjwa kusafirisha wagonjwa walioambukizwa virusi vya ugonjwa wa Covid-19 kwenye lango la hospitali ya Daegu Februari 23, 2020. Kesi 602 za maambukizi na vifo 5 vyathibitishwa Korea Kusini.
Wafanyakazi wa afya wakisubiri gari ya wagonjwa kusafirisha wagonjwa walioambukizwa virusi vya ugonjwa wa Covid-19 kwenye lango la hospitali ya Daegu Februari 23, 2020. Kesi 602 za maambukizi na vifo 5 vyathibitishwa Korea Kusini. YONHAP / AFP
Matangazo ya kibiashara

Korea Kusini ndio eneo muhimu zaidi la maambukizi nje ya China Bara ambapo ugonjwa huo ulianzia mwezi Desemba.

Uamuzi huo wa kuahirisha mazoezi hayo ya pamoja ya kijeshi umetolewa baada ya Seoul kutangaza kiwango cha juu cha tahadhari kuhusu "virusi" hivyo, uongozi wa pamoja wa kijeshi umesema katika taarifa yake Alhamisi wiki hii, na kuongeza kuwa mazoezi ya kijeshi nchini Korea Kusini yameahirishwa.

Marekani ina askari 28,500 nchini Korea Kusini ili kulinda nchi hii ya Mashariki ya Mbali dhidi ya jirani yake, Korea Kaskazini, ambayo ina silaha za nyuklia.

Wanajeshi wengi wamewekwa katika kambi ya Humphreys huko Pyeongtaek, kambi kubwa zaidi ya kijeshi ya Amerika nje ya nchi hiyo.

Nchi hizo mbili tayari zimepunguza mazoezi yao ya kijeshi kwa kuwezesha mazungumzo juu ya mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini - ambayo inalaani mara kwa mara mazoezi hayo ya kijeshi ambayo inayaona kama mwanzo wa uvamizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.