Pata taarifa kuu

Nigeria: Wanafunzi 137 walioachiliwa wameunganishwa tena na familia zao

Wanafunzi 137 waliotekwa nyara mnamo Machi 7 na magenge yenye silaha kaskazini-magharibi mwa Nigeria na kuachiliwa Jumapili wanatarajiwa kurejeshwa makwao siku ya Alhamisi baada ya kupata matibabu na kuunganishwa na wapendwa wao, ametangaza msemaji wa gavana wa jimbo la Kaduna.

Wakazi wa kijiji cha Tantatu katika wilaya ya Kajuru Station Machi 19, 2024.
Wakazi wa kijiji cha Tantatu katika wilaya ya Kajuru Station Machi 19, 2024. Β© AFP
Matangazo ya kibiashara

Watoto hao, kutoka sekta ya Kuriga, walifanyiwa uchunguzi wa kimatibabu katika mji mkuu wa mkoa wa Kaduna, ambapo waliunganishwa tena na wapendwa wao.

"Zoezi hili limeleta shauku kubwa," amesema msemaji wa Gavana wa jimbo la Kaduna, Muhammad Shehu, akiongeza kuwa watoto hao walipaswa kurejea nyumbani siku ya Alhamisi.

Sita kati yao walilazimika kulazwa hospitalini ili kutibu majeraha waliyoyapata wakiwa kifungoni. Mtu mzima aliyetekwa nyara na kundi la watoto alifariki, kulingana na mamlaka.

Mnamo Machi 7, makumi ya watu waliokuwa na silaha walivamia shule moja huko Kuriga, na kuwachukua kwa nguvu wanafunzi na mtu mzima huyu.

Makadirio ya awali yaliripoti zaidi ya wanafunzi 280 waliotekwa nyara, kabla ya idadi hiyo kupunguzwa hadi watoto 137, wasichana 76 na wavulana 61.

Nigeria, ambayo inakabiliwa na mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 30, inakabiliwa na ongezeko la utekaji nyara ili kulipwa fidia.

Malipo ya fidia Β yamepigwa marufuku rasmi tangu sheria iliyopitishwa mwaka wa 2022 na mamlaka inakataa malipo yoyote wakati mateka wanapoachiliwa kufuatia mazungumzo na watekaji nyara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.