Pata taarifa kuu

Nigeria: Rais Tinubu ameunda kikosi kazi cha kutafuta suluhu ya uchumi wa nchi

Nairobi – Rais wa Nigeria Bola Tinubu ametangaza kuundwa kwa kikosi kazi  cha dharura chenye jukumu la kujaribu kutafuta suluhu ya uchumi wa nchi hiyo unaoendelea kushuka.

Rais wa Nigeria Bola Tinubu.
Rais wa Nigeria Bola Tinubu. REUTERS - TEMILADE ADELAJA
Matangazo ya kibiashara

Bei za vyakula na bidhaa za mafuta zimeripotiwa  kupanda, idadi kubwa ya raia wakionekana kukabiliwa na changamoto kutokana na mishahara yao midogo.

Matatizo makubwa ya kiuchumi yamechangia ugumu wa maisha hatua ambayo imeendelea kutoa shinikizo kubwa kwa utawala wa rais Tinubu kutafuta suluhu ya tatizo hilo.

Baadhi ya raia wa Nigeria wameituhumu serikali  kwa kuondoa ruzuku ya mafuta , hatua ambayo imechangia kushuka kwa thamani ya sarafu ya nchi hiyo ,naira suala ambalo pia limetajwa kuchangia kupanda kwa gharama ya maisha.

Kikosi kazi hicho kinaundwa na maafisa wakuu wa serikali na viongozi wenye tajiriba katika nyanja tofauti.

Rais pia alianzisha baraza la rais la uratibu wa uchumi (PECC) ambalo atakuwa mwenyekiti na kusimamia mageuzi ya kiuchumi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.