Pata taarifa kuu
ADHABU YA KIFO

DRC yarejesha utekelezaji wa adhabu ya kifo

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetangaza kumalizika kwa usitishaji wa adhabu ya kifo, na hivyo kutoa mwanya wa kuanza kutekelezwa kwa adhabu hiyo nchini humo.

Mnamo Februari 5, Baraza la Juu la Ulinzi lilimtaka Félix Tshisekedi "kufuta sheria ya kusitishwa kwa utekelezaji wa adhabu ya kifo, kuhusiana na maswali ya usaliti ndani ya vikosi vya ulinzi na usalama".
Mnamo Februari 5, Baraza la Juu la Ulinzi lilimtaka Félix Tshisekedi "kufuta sheria ya kusitishwa kwa utekelezaji wa adhabu ya kifo, kuhusiana na maswali ya usaliti ndani ya vikosi vya ulinzi na usalama". AFP PHOTO / FEDERICO SCOPPA
Matangazo ya kibiashara

Adhabu ya kifo inaweza kutekelezwa hasa dhidi ya askari wenye hatia ya uhaini na wahalifu wa "ujambazi wa mjini unaosababisha kifo cha mtu yeyote".

Uamuzi huu, ulioarifiwa katika waraka uliotiwa saini siku ya Jumatano na Waziri wa Sheria Rose Mutombo, unafuta sheria ya kusitishwa kwa utekelezaji wa hukumu ya kifo ya mwaa 2003, nakala hii inabainisha.

Taarifa hili imeelekezwa kwa wakuu wa taasisi akiwemo rais wa Baraza la Juu la Mahakama na rais wa Mahakama ya Katiba, rais wa kwanza wa Mahakama ya Juu, mwendesha mashtaka mkuu katika Mahakama hii, rais wa kwanza wa Mahakama Kuu ya Kijeshi, pamoja na mkaguzi mkuu wa FARDC.

Katika utekelezaji wa uamuzi huu, adhabu ya kifo kufuatia hukumu ya mahakama isiyoweza kubatilishwa inayotokea wakati wa vita, chini ya hali ya kuzingirwa au dharura, wakati wa operesheni ya polisi inayolenga kudumisha au kurejesha utulivu wa umma au wakati wa hali nyingine yoyote ya kipekee, itatumika, inabaini taarifa hii kutoka kwa Waziri wa Sheria.

Hii ni kwa mujibu wa baadhi ya Ibara za sheria zinazohusiana na makosa yanayohusiana na adhabu ya kifo, hususan kushirikiana na wahalifu, uhaini, ujasusi, ushiriki katika magenge yenye silaha, kushiriki katika makundi ya waasi, kwa mujibu wa kitabu cha II cha jinai.

Imeongezwa kwa haya ni uhalifu wa kivita, uhalifu wa mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu, vifungu vinavyoangukia chini ya sheria ya Januari 30, 1940 iliyoanzisha Kanuni ya Adhabu. Pia kutoroka jeshi na kwenda upande wa adui,  kuhatarisha usalama wa taifa, njama za kijeshi, kukataa kutii na kukataa kupambana dhidi ya adui, ukiukaji wa maagizo mbele ya adui au genge lenye silaha.

Pia kuna kujiepusha kwa hiari kwa kamanda wa kitengo kutimiza dhamira inayohusiana na operesheni za vita ambayo ameshtakiwa, kutelekeza ngome mbele ya adui, hujuma inayofanywa kwa maslahi ya nchi ya kigeni, wizi, matumizi mabaya na uharibifu mbaya ni makosa yote yaliyoainishwa na Kanuni ya Adhabu ya Kijeshi.

Ni tangu mwaka 2003 ambapo adhabu ya kifo haijatekelezwa tena nchini DRC, ingawa imetamkwa na mahakama hasa za kijeshi, haswa kwa sababu ya kusitishwa kwa utekelezaji kama huo ambao umefutwa kwa sasa. 

Mnamo Februari 5, Baraza la Juu la Ulinzi lilimtaka Félix Tshisekedi "kufuta sheria ya kusitishwa kwa utekelezaji wa adhabu ya kifo, kuhusiana na maswali ya usaliti ndani ya vikosi vya ulinzi na usalama".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.