Pata taarifa kuu

DRC: Mbunge wa zamani Janet Kabila ameitwa kwenye idara ya kijasusi ya kijeshi

Nairobi – Katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mbunge wa zamani Janet Kabila, dada pacha wa rais wa zamani Joseph Kabila, ameitwa kwenye idara ya kijasusi ya kijeshi. Wito ambao unakuja baada ya idara ya ujasusi ya jeshi la Kongo kupekua makao makuu ya taasisi inayoongozwa na Janet Kabila na ambayo ina jina la babake, rais wa zamani aliyeuawa mwaka 2001.

Wakfu wa Laurent Désiré Kabila
Wakfu wa Laurent Désiré Kabila © Junior D. Kannah / AFP
Matangazo ya kibiashara

Barua hiyo imemtaka pacha wa rais Joseph Kabila mbunge wa zamani Janet Kabila kuwasili kwenye idara ya ujasusi wa kijeshi kwa ajili ya taarifa punde tu baada ya kupokea muamiko huo. Mualiko uliosaini na mkuu wa idara ya ujasusi wa kijeshi meja jenerali Ndayiwel Ekura Christian.

Janet Kabila ambaye yuko jijini Kinshasa hakupenda kuzungumzia mualiko huo lakini watu wake wa karibu wanasema huu ni uchokozi usiokubalika. kwa mujibu wa taarifa iliosainiwa na Janet Kabila wanajeshi walivamia makao makuu ya taasisi ya mzee Laurent Desire Kabila mchana kweupe na kuondoka na kampyuta, simu na vifaa vingine muhimu vyanye thamani huku walinzi watatu na maafisa wawili wa taasisi wamekamatwa.

Taarifa zaidi zinasema wanajeshi  waliondoka na gari lililobeba maiti ya hayati Mzee Laurent Deisire kabisa wakati wa mazishi yake mwaka 2001. tangu miaka miwili, makao makuu ya taasisi hiyo yamekuwa yakitembelewa na maafisa wa uslama mara kwa mara. Hata hivyo viongozi wa serikali hawajazungumzia lolote kuhusu tukio hili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.