Pata taarifa kuu

DRC : Mkurugenzi wa ANR na manaibu wake 2 wakamatwa kwa madai ya kushirikiana na M23

Mkurugenzi wa idara ya jasusi (ANR) katika mkoa wa Kivu Kaskazini, manaibu wake wawili na msemaji wa kiraia wa gavana wa mkoa huo wanazuiliwa mjini Kinshasa baada ya kukamatwa huko Goma tangu siku ya Jumanne Februari 13.

Wanajeshi wa DRC waimarisha ngome zao karibu na mji wa Goma katika siku ya pili ya mapigano dhidi ya waasi wa M23.
Wanajeshi wa DRC waimarisha ngome zao karibu na mji wa Goma katika siku ya pili ya mapigano dhidi ya waasi wa M23. © MONUSCO
Matangazo ya kibiashara

 

Kurugenzi Kuu ya Ujasusi wa Kijeshi inawashutumu kwa madai ya kuhusika na uasi wa M23, unaoungwa mkono na Rwanda, kulingana na Radio OKAPI inayorusha matangazo yake nchini DRC.

Kitengo hiki cha jeshi la taifa kinadai kuwa kilifanya hivyo baada ya kunasa mawasiliano kati ya watuhumiwa na waasi wa M23.

Msemaji mpya wa kiraia wa gavana wa kijeshi wa mkoa wa Kivu Kaskazini, ambaye alikuwa ameteuliwa wiki chache zilizopita, alikuwa kada wa chama cha kisiasa cha Corneille Nangaa, na alijiondoa katika chama hicho muda mfupi kabla ya uchaguzi.

Alipohojiwa kuhusu suala hili, msemaji wa kijeshi wa Gavana wa Kivu Kaskazini, Luteni Kanali Njike Kaiko amesema bila maelezo zaidi kuwa faili hili liko mikononi mwa mahakama.

Kukamatwa huku kulifanyika wakati mapigano yakiendelea kati ya FARDC, wanamgambo wa ndani na waasi wa M23, wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda, katika maeneo ya Sake, huko Masisi (Kivu Kaskazini).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.