Pata taarifa kuu

RDC: Wanajeshi wa serikali wadhibiti hali katika mji wa Masisi

Nairobi – Hali ya utulivu imeshuhudiwa jana Alhamisi Februari 15, 2024, kwenye karibu ngome zote za mapigano katika eneo la Masisi -Kivu Kaskazini.

FARDC, inaungwa mkono na vijana wazalendo, ambao wameendelea kudhibiti ngome zao huko Sake
FARDC, inaungwa mkono na vijana wazalendo, ambao wameendelea kudhibiti ngome zao huko Sake AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

FARDC, inayoungwa mkono na vijana wazalendo, ambao wameendelea kudhibiti ngome zao huko Sake na Bweremana karibu na Shasha mji unaokaliwa na waasi wa M23/RDF tangu juma lililopita.

Kukaliwa kwa mji wa Shasha na kundi la M23/RDF kumesababishwa kusitishwa kwa shughuli za usafiri kati ya Sake na Minova barabara pekee iliokuwa imesalia kusambaza chakula na bidhaa nyingine kwenda Goma.

Waasi wa M23 wanadaiwa na serikali ya kinshasa kuungwa mkono na Rwanda
Waasi wa M23 wanadaiwa na serikali ya kinshasa kuungwa mkono na Rwanda REUTERS - JAMES AKENA

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa mashirika ya kiraia huko Masisi, Voltaire Batundi, hali bado haitabiriki, baada ya mapigano hayo kuripotiwa siku ya Jumatano, kwenye milima inavyoutazama mji wa Shasha.

Wakati huo huo, idadi ya watu waliokimbia makazi yao imeendelea kuongezeka katika maeneo mbalimbali huko huko Goma, haswa huko Bulengo, iliyoko katika wilaya ya Lac Vert, magharibi mwa jiji.

Maelfu ya wakaazi wa mashariki mwa DRC wanakabiliwa na changamoto za kiusalama wengi wakitoroka makazi yao
Maelfu ya wakaazi wa mashariki mwa DRC wanakabiliwa na changamoto za kiusalama wengi wakitoroka makazi yao AFP - AUBIN MUKONI

Watu hawa waliolazimishwa kukimbia wanatoka hasa Shasha, Sake na maeneo ya jirani.

Wanakimbia mapigano mapya, ambayo yamezuka hivi karibuni kati ya FARDC, inayoungwa mkono na Wazalendo, na waasi wa 23/ wanaoungwa mkono na jeshi la Rwanda

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.