Pata taarifa kuu

Rais Sall kulihutubia taifa, katikati ya mjadala wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais

Rais wa Senegal Macky Sall atalihutubia taifa siku ya Jumamosi, kulingana na shirika la habari la AFP likinukuu chanzo kutoa ofisi ya rais, katikati ya mjadala wa kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais wa Februari 25.

Rais wa Senegal Macky Sall katika Mkutano Mkuu wa 78 wa Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Septemba 19, 2023.
Rais wa Senegal Macky Sall katika Mkutano Mkuu wa 78 wa Umoja wa Mataifa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa huko New York, Septemba 19, 2023. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Hotuba ya Rais Sall imepangwa saa 12:00 GMT sawa na saa za ndani, vyanzo viwili katika ofisi ya rais wa Senegal vimeliambia shitika la habari la AFP, bila maelezo zaidi.

Ujumbe wa kiongozi huyo wa Senegal umewekwa saa chache kabla ya kufunguliwa kwa kampeni za uchaguzi wa Februari 25, uliopangwa kufanyika Jumamosi usiku wa manane, ambapo wagombea 20 wameidhinishwa na Baraza la Katiba.

Rais Sall, aliyechaguliwa mnamo 2012 kwa miaka saba na kuchaguliwa tena mnamo 2019 kwa miaka mitano, alitangaza mnamo Julai kwamba hatawania katika uchaguzi huo wa urais.

Baraza la Katiba liliwaondoa wagombea kadhaa katika uchaguzi huo, wakiwemo viongozi wawili wa upinzani, mgombea anayepinga mfumo Ousmane Sonko na Karim Wade, waziri na mtoto wa rais wa zamani Abdoulaye Wade (2000-2012).

Siku ya Jumatano, Bunge la taifa liliidhinisha, baada ya mijadala yenye misukosuko, kuundwa kwa tume ya kuchunguza mchakato huo. Idadi kubwa ya wanachama wa kambi ya rais walipiga kura "Ndio".

Msaada huu umezusha matatizo. Wapinzani wa rais anayeondoka wanashuku mpango wa kuahirisha uchaguzi wa urais kwa sababu walio mamlakani wanahofia kushindwa. Baraza la Katiba ni chombo muhimu katika mchakato wa uchaguzi. Limetakiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa urais na kutoa uamuzi kuhusu mizozo inayoweza kutokea.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Thérèse Faye, pia kiongozi wa kambi ya rais, alizungumza Ijumaa akiunga mkono kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais kwa angalau miezi sita.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Thérèse Faye, ametangaza kwenye televisheni ya kibinafsi ya TFM kwamba mchakato wa uchaguzi ambao ulipelekea mwezi wa Januari kuidhinishwa kwa wagombea 20 na Baraza la Katiba "umevurugwa" na dosari.

"Nina unga mkono kuahirishwa kwa uchaguzi wa urais kwa angalau miezi sita," amesema Bi. Faye, ambaye hata hivyo ni afisa katika chama cha rais anayejulikana kuwa karibu na mkuu wa nchi Macky Sall. Amesema anataka "uchaguzi wa urais shirikishi na usiyomtenga mtu yeyote".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.