Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Senegal: Mahakama yafutilia mbali hoja ya kumuachilia huru Bassirou Diomaye Faye

Mahakama nchini Senegal imekataa ombi la kuachiliwa kwa mgombea anayeziliwa jela Bassirou Diomaye Faye wakati kampeni ya uchaguzi wa urais inaanza Jumapili, kulingana na kambi ya mwanasiasa huyo wa upinzani. Kulingana na shirika la habari la AFP,  halijapata uthibitisho wa kukataa huku kutoka kwa wanasheria wake.

Bw. Faye anazuiliwa jela tangu mwaka 2023. Hata hivyo anaonekana kuwa anaweza kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais.
Bw. Faye anazuiliwa jela tangu mwaka 2023. Hata hivyo anaonekana kuwa anaweza kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais. © Bassirou Diomaye Faye
Matangazo ya kibiashara

 

Bw. Faye aliwasilisha ombi la kuachiliwa kwa muda mnamo Januari 22, siku mbili baada ya kuchapishwa kwa orodha ya mwisho ya wagombea urais na Baraza la Katiba (Mahakama ya Katiba) na kuthibitishwa kwa kuwania kwake, inabainisha taarifa kutoka kwa muungano wa "Diomaye président" iliyotolewa siku ya Jumatano jioni. Lakini siku ya Jumanne jaji aliamuru ombi hilo kutupiliwa mbali, imesema taarifa hiyo.

"Utawala unaendelea na nia yake ya kuvunja haki za mwanasiasa yoeyote wa upinzani," taarifa imesema. Serikali mara kwa mara hujitete dhidi ya kuingiliwa kwa aina yoyote katika masuala ya mahakama. "Kwa mara ya kwanza katika historia yetu mgombea anayeshtumiwa na hata hajahukumiwa, kwa hivyo ambaye bado ana haki zake za kisiasa, anazuiwa kufanya kampeni," imesema taarifa hiyo .

Mahakama ilikataa maombi kadhaa ya awali ya kuachiliwa. Masharti ambayo Bw. Faye atatetea hoja yake ni mojawapo ya mambo yasiyojulikana ya kampeni hiyo inayoanza rasmi siku ya Jumapili.

Bw. Faye anazuiliwa jela tangu mwaka 2023. Hata hivyo anaonekana kuwa anaweza kuibuka mshindi katika uchaguzi wa urais. Chama kilichovunjwa cha Pastef, ambacho yeye ni katibu mkuu, kilimchagua kuchukua nafasi ya kiongozi wake Ousmane Sonko, aliyefungwa mwaka 2023 baada ya zaidi ya miaka miwili ya mzozo na mamlaka ambayo yalizua machafuko mabaya.

Baraza la Kikatiba lilitaja kuwa Bw. Sonko hstahili kugombea katika uchaguzi wa urais. Ujumbe uliotumwa na Umoja wa Ulaya nchini Senegal kuangalia uchaguzi wa rais uliona kuwa ni "muhimu sana" siku ya Jumatano kwamba Bw. Faye anaweza kufanya kampeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.