Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-DEMOKRASIA

Marekani yaitaka Senegal 'haraka' kutangaza tarehe mpya ya uchaguzi wa urais

Marekani imetangaza kuwa "ina wasiwasi mkubwa" siku ya Jumamosi kwa tangazo la kuahirishwa kwa muda usiojulikana kwa uchaguzi wa urais nchini Senegal na kuzitaka mamlaka kupanga tarehe mpya "haraka na kwa utulivu".

Mpita njia akipita katika moja ya maeneo ya mki mkuu wa Senegal, Dakar,  mnamo Juni 3, 2023, kulikoripotiwa ghasia mbaya katika mji mkuu wa Senegal.
Mpita njia akipita katika moja ya maeneo ya mki mkuu wa Senegal, Dakar, mnamo Juni 3, 2023, kulikoripotiwa ghasia mbaya katika mji mkuu wa Senegal. Β© Seyllou / AFP
Matangazo ya kibiashara

Β 

"Tunawaomba washiriki wote katika mchakato wa uchaguzi wa Senegal kushiriki kwa amani katika juhudi muhimu zinazolenga kupanga kwa haraka tarehe mpya na mazingira ya uchaguzi huru na wa haki," Ofisi ya Masuala ya Afrika katika wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani imeandika kwenye mtandao wa X (zamani ikiitwa Twitter), na kuongeza kuwa Senegal "ina utamaduni thabiti wa demokrasia na kukabidhiana madaraka kwa amani ."

Hayo yanajiri wakati Rais wa Senegal Macky Sall, anayemaliza muda wake, ametangaza kuwa uchaguzi mkuu uliokuwa umepangwa kufanyika tarehe 25 mwezi huu, umeahirishwa kwa muda usiojulikana.

Akilihotubia taifa siku ya Jumamosi, rais Sall amesema ametia saini hati ya kuahirishwa Β kwa uchaguzi huo na kuagiza wabunge kuwachunguza Majaji mawili Baraza la Katiba baada ya sifa zao za utendaji kutiliwa shaka kufuatia zoezi la kuwapata wagombea wa urais.

Hatua hii imekuja baada ya chama Senegalese Democratic Party (PDS) Β chake rais wa zamani Abdoulaye Wade, siku ya Ijumaa kuwasilisha mswada bungeni kutaka uchaguzi huo uahirishwe kwa madai kuwa, mazingira yaliyopo yanatilia shaka, uchaguzi huo kuwa huru na haki.

Mgombea wa chama hiki Karim Wade, alizuiwa kuwa miongoni mwa wagombea 20 waliopitishwa na Baraza la Katiba baada ya kubainika kuwa alikuwa hajafuta uraia wake wa Ufaransa.

Hata hivyo, baadhi ya wanasiasa wakiongozwa na mmoja wa wagombea Khalifa Sall, amekuwa akipinga mapendekezo ya uchaguzi huo kuahirishwa kwa madai kuwa iwapo utaahirishwa, utavuruga hali ya kisiasa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.