Pata taarifa kuu

DRC inamkumbuka shujaa wake aliyetetea uhuru Patrice-Emery Lumumba

DRC inaadhimisha Jumatano hii, Januari 17, kifo cha Waziri Mkuu wa kwanza wa Kongo, Patrice-Emery Lumumba, aliyeuawa miaka 63 iliyopita huko Élisabethville (leo Lubumbashi), huko Katanga.

Mtetezi wa uhuru wa Congo (DRC) Patrice-Emery Lumumba mnamo mwaka 1960.
Mtetezi wa uhuru wa Congo (DRC) Patrice-Emery Lumumba mnamo mwaka 1960. © AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Mmoja wa wababa wa uhuru wa Kongo, Lumumba pia ni mfano wa uhuru wa Afrika.

Hotuba aliyoitoa Juni 30, 1960, wakati wa sherehe za kusherehekea uhuru wa iliyokuwa Kongo ya Ubelgiji (Congo-belge), ilibaki katika kumbukumbu.

Lumumba anakumbuka mapambano ya muda mrefu, "ya moto na ya kimawazo" ya watu wa Kongo kufikia uhuru.

"Zaidi ya miaka 60 baada ya kifo chake, Lumumba bado anajumuisha, zaidi ya hapo awali, wazo la taifa kubwa la Kongo ambalo alitaka kuwa na nguvu, moja na isiyoweza kugawanyika," mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Denis Mukwege alimzngumzia mnamo Juni 30, 2023.

Patrice-Emery Lumumba alipigania Kongo yenye nguvu katika moyo wa Afrika na kichocheo cha maendeleo ya bara letu, alisisitiza.

Akimtaja shujaa huyu wa kitaifa, Profesa Justin Haguma, daktari wa historia, alitangaza mnamo Januari 15, 2023:

“Mashujaa wetu wa kitaifa ni urithi wetu. Uwepo wao unajumuisha kwa watu wote mbolea ambayo inaweza kuotesha mafanikio ya kishujaa leo. Ili kufanya hivi, lazima tufanikiwe kujenga uzalendo katika msingi wa itikadi za utaifa za Laurent-Désiré Kabila na Patrice-Emery Lumumba.”

Kulingana na Redio Okapi inayosikika nchini DRC, ikimnukuu Profesa Blaise Muya, mkuu wa Chuo Kikuu cha Simon Kimbangu cha Kinshasa (USK), “Patrice Emery Lumumba aliendeleza vita vya Simon Kimbagu vya kutafuta uhuru si tu kisiasa bali pia kiroho. Simon Kimbangu alikuwa ametayarisha mazingira kwa Lumumba kuja kumuendeleza Laurent-Désiré Kabila.”

Tangu Juni 30, 2022, baadhi ya viungo hususan jino la Patrice-Emery Lumumba, lililorejeshwa siku chache mapema kutoka Ubelgiji, lipo kwenye kaburi lililojengwa kwa minajili yake huko Limete/Kinshasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.