Pata taarifa kuu

Rwanda yadai kumuua 'mwanajeshi' wa DRC na kuwakamata wengine wawili mpakani

Jeshi la Rwanda limedai mnamo Januari 16, 2024 kumuua "askari" kutoka DRC na kuwakamata wengine wawili ambao, kulingana na Kigali, walivuka mpaka kati ya nchi hizo mbili.

[Picha ya kielelezo] Wanajeshi wa Rwanda wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) na maafisa wa polisi wa Rwanda wanajiandaa kupanda ndege ya “Rwandair” kwa misheni ya kijeshi nchini Msumbiji, Julai 10, 2021.
[Picha ya kielelezo] Wanajeshi wa Rwanda wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) na maafisa wa polisi wa Rwanda wanajiandaa kupanda ndege ya “Rwandair” kwa misheni ya kijeshi nchini Msumbiji, Julai 10, 2021. AFP - SIMON WOHLFAHRT
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kigali, Lucie Mouillaud

Tukio jipya lililotokea mpakani kati ya Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kulingana na jeshi la Rwanda. RADF inathibitisha Januari 16, 2024 kwamba askari watatu wa Kongo waliingia kwenye ardhi ya Rwanda baada ya kuvuka mpaka wa nchi hizo mbili, wawili walikamatwa na mmoja aliangamzwa.

Kwa mujibu wa Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF), tukio hilo lilitokea mwendo wa saa 1:10 asubuhi saa za Kigali Jumanne asubuhi. Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari, wanajeshi watatu wa Kongo wenye silaha walivuka mpaka katika wilaya ya Rubavu, kwa usahihi zaidi katika eneo la Rukoko, linalopakana na mkoa wa Kivu Kaskazini nchini DRC na karibu sana na mji wa Goma.

Matukio na uvamizi

Miongoni mwao, sajenti na koplo, wote walikamatwa na doria ya Rwanda na mtandao wa ulinzi wa jirani. Kulingana na RDF, mwanajeshi wa tatu wa Kongo aliuawa kwa kupigwa risasi, wakati aliwafyatulia risasi askari walipowataka wajisalimishe.

Tukio ambalo linatokea katika hali ya mvutano kwa miaka miwili kati ya nchi hizo mbili. Kinshasa hasa inaishutumu Kigali kwa kupeleka wanajeshi katika mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Kongo kusaidia kundi la waasi la M23, shutuma ambazo bado zinakanushwa na Rwanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.