Pata taarifa kuu

Senegal: Wagombea 28 nadai uwazi zaidi juu ya udhibiti wa udhamini

Nchini Senegal, wakati duru ya pili na ya mwisho ya kuwapata wagombea 23 katika uchaguzi wa urais inaanza leo, muungano wa wagombea 28 wanadai hatua za haraka za kurekebisha mfumo wa udhibiti wa udhamini. Jana walikata rufaa rasmi mbele ya Baraza la Wazee wa Busara.

Aminata Touré na Ousmane Sonko, wagombea katika uchaguzi wa urais, wanashindana na wapinzani wengine 26, wanasema hawana imani na mfumo wa udhibiti wa ufadhili kwa uchaguzi wa urais.
Aminata Touré na Ousmane Sonko, wagombea katika uchaguzi wa urais, wanashindana na wapinzani wengine 26, wanasema hawana imani na mfumo wa udhibiti wa ufadhili kwa uchaguzi wa urais. © Mamadou Gomis Reuters & Sylvain Cherkaoui AP
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa habari huko Dakar, Léa-Lisa Westerhoff

Ukosoaji mkuu wa watia saini 28 wa ombi hilo, ikiwa ni pamoja na mpinzani Ousmane Sonko, lakini pia Waziri Mkuu wa zamani Aminata Touré: kubatilishwa kwa maelfu ya wafadhili wa faili zao za maombi kwa sababu "haijatambuliwa" na Baraza la Wazee basi wakati watu hawa walisajiliwa kwenye daftari la uchaguzi kama ilivyoelezwa na Aly Ngouille Ndiaye, waziri wa zamani na mgombea ambaye anakemea tatizo kubwa: "Nilikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Senegal, ni mimi niliyepanga uchaguzi wa mwaka 2019, kwa hivyo najua kile ninachokuzungumzia. Ni jambo la kawaida kwetu kuuliza maswali kwa sababu mtu anapokuwa na kadi yake ya kupiga kura, anaandikwa, na hajawahi kubadilisha kituo chake cha kupigia kura, hakuna kinachoweza kuhalalisha kutokuwa katika kituo cha kupigia kura. "

Naye Waziri Mkuu wa zamani Aminata Touré anasema maelfu haya ya watu kwaliokosekana bila maelezokwenye daftari la uchaguzi, watu 10,000, ni jambo ambalo linatia shaka juu ya mtu kuwa na imani na mfumo wa udhibiti wa ufadhili na daftari la uchaguzi linalotumiwa na Baraza la Katiba: "Ni mara ya kwanza katika historia ya Senegal. Katika suala la ujazo, swali tunalojiuliza ni faili gani tuzingatie, Baraza la Katiba linatumia faili gani kudhibiti udhamini? »

Watia saini 28 wanaomba Baraza la Katiba lirekebishe makosa haya na kuwa wazi zaidi kwenye faili ya uchaguzi au programu ambayo hutumiwa kuhakiki udhamini ili kila mtu ajue kinachoendelea.

Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, Baraza la Katiba lilijiwekea kikomo kwa kutoa orodha ya wagombea 23 waliokubaliwa kuhalalisha ufadhili wao ambao haujaidhinishwa ndani ya saa 48.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.