Pata taarifa kuu

Senegal: Uchunguzi wa faili za wagombea kwa uchaguzi wa rais waendelea

Wiki iliyopita, baadhi ya wagombea waliidhinisha ufadhili wao kama vile Waziri Mkuu Amadou Ba au wapinzani Khalifa Sall na Karim Wade. Wengine lazima warekebishe orodha yao ya wafadhili, na wengine wameondolewa moja kwa moja.

Maahakama ya Katiba ina hadi Januari 12 kumaliza kukagua ufadhili, kisha hadi Januari 20 kuchunguza hati zingine zote pamoja na rekodi ya uhalifu na hali ya ushuru.
Maahakama ya Katiba ina hadi Januari 12 kumaliza kukagua ufadhili, kisha hadi Januari 20 kuchunguza hati zingine zote pamoja na rekodi ya uhalifu na hali ya ushuru. William de Lesseux/RFI
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Dakar, Juliette Dubois

Kati ya faili tisini na tatu zilizowasilishwa, ni tisa pekee ndizo zilizoidhinisha ufadhili wao wiki iliyopita. Wagombea ishirini watapitia raundi ya pili ya ukaguzi.

Jambo linalohusika: uwepo kwenye fomu yao ya udhamini ya nakala za nje, yaani, majina ambayo yalikuwepo kwenye fomu ya mgombea mmoja au zaidi, pamoja na majina ambayo hayapo kwenye daftari ya uchaguzi. Iliarifiwa Ijumaa, wagombea wanaohusika wana hadi saa 5 asubuhi Jumatatu hii kuleta orodha mpya kwenye Baraza la Katiba.

Kwa wengine, inapaswa kuwa rahisi kupata saini zinazokosekana, kama kwa Malick Gakou wa chama cha Grand Party ambaye amekosewa na karibu saini 3,500 kati ya 44,000 walizoombwa, au Idrissa Seck, Waziri Mkuu wa zamani, ambaye alilazimika kutafuta chini kidogo ya saini 6,000.

Kwa wengine, ucheleweshaji huo ni muhimu zaidi, hii ni kesi ya daktari wa uzazi Rose Wardini ambaye lazima aweke sawa majina 31,000. Au hata Waziri Mkuu wa zamani Aminata Touré aliye na wafadhili 19,000 ambao hawakuwa halali.

Wagombea wengi walikataliwa moja kwa moja, kwa sababu ya kukosekana kwa hati kwenye faili au idadi isiyotosha ya wafadhili. Miongoni mwao, watu wenye ushawishi kama Waziri Mkuu wa zamani Cheikh Hadjibou Soumaré, kaka yake Rais Macky Sall Adama Faye, Aida Mbodj, waziri wa zamani na mpinzani Ousmane Sonko.

Baraza la Katiba (Mahakaam ya Katiba) lina hadi Januari 12 kumaliza kukagua ufadhili, kisha hadi Januari 20 kuchunguza hati zingine zote pamoja na rekodi ya uhalifu na hali ya ushuru.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.