Pata taarifa kuu

Watoto wa Sudan waliokimbilia nchini Chad wako katika hatari ya kupata utapiamlo

Maelfu ya watoto kutoka familia waliotoroka Sudan inayokumbwa na vita na kukimbilia nchini Chad wako katika hali "ya wasiwasi" ya kupata utapiamlo, Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limeonya siku ya Ijumaa, likitoa wito wa "msaada wa dharura wa chakula."

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) pia "linaonya juu ya hatari ya kuwekewa vikwazo au kusitisha sehemu ya shughuli zake nchini Chad kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha", pia MSF ambayo inatiwa hofu, inaitaka jumuiya ya kimataifa "kuimarisha" msaada wa dharura wa chakula'.
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) pia "linaonya juu ya hatari ya kuwekewa vikwazo au kusitisha sehemu ya shughuli zake nchini Chad kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha", pia MSF ambayo inatiwa hofu, inaitaka jumuiya ya kimataifa "kuimarisha" msaada wa dharura wa chakula'. REUTERS - ZOHRA BENSEMRA
Matangazo ya kibiashara

Chad, ambayo tayari inawapa hifadhi idadi kubwa zaidi ya wakimbizi wa Sudan, karibu 900,000, ilipokea zaidi ya wakimbizi 8,000 wapya katika wiki ya kwanza ya mwezi Novemba pekee, kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).

Idadi hii iliongezeka katika wiki za hivi karibuni kutoka Darfur, jimbo la Sudan linalopakana na mashariki mwa Chad, eneo linalokumbwa na "machafuko makubwa" kulingana na Umoja wa Mataifa, ambao hivi karibuni ulisema unahofia uwezekano wa kutokea "mauaji mapya ya halaiki" huko Darfur.

Katika moja ya kambi hizi zenye watu 40,000, ile ya Metché, MSF imerekodi "kiwango cha maambukizi ya kupita kiasi ya 13.6% kati ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano", kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari. Mwezi Agosti na Septemba, MSF ilirekodi viwango vikali vya utapiamlo vya 4.8% na 4.6%, ambavyo tayari vilikuwa "mara mbili ya kizingiti cha dharura kilichoamuliwa na Shirika la Afya Duniani (WHO)." , inaeleza taarifa hiyo.

"Timu za MSF zimehudumia takriban watoto 14,000 wenye utapiamlo katika (...) programu tofauti za wagonjwa wa nje" tangu mwanzo wa mwaka, ambao "karibu 3,000 (...) walilazimika kulazwa hospitalini wakiwa katika hali mbaya", shirika hili limebainisha . "Kwa hakika, hii ina maana kwamba watoto ambao walinusurika dhulma, mashambulizi ya mara kwa mara na ghasia kali ambazo ziliikumba Darfur, sasa wanajikuta katika hali ya wasiwasi ya kiafya nchini Chad," linaunga mkono shirika hilo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) pia "linaonya juu ya hatari ya kuwekewa vikwazo au kusitisha sehemu ya shughuli zake nchini Chad kutokana na ukosefu wa fedha za kutosha", pia MSF ambayo inatiwa hofu, inaitaka jumuiya ya kimataifa "kuimarisha" msaada wa dharura wa chakula'.

Sudan imesambaratika tangu katikati ya mwezi wa Aprili kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mkuu wa jeshi na mtawala mkuu wa nchi hiyo, Jenerali Abdel Fattah al-Burhane, na aliyekuwa mshirika wake wa karibu Jenerali Mohamed Hamdane Daglo.

Mgogoro huu hadi sasa umesababisha zaidi ya vifo 10,400, kulingana na makadirio ya shirika lisilo la kiserikali la Armed Conflict Location & Event Data Project (ACLED), na kusababisha zaidi ya watu milioni 4.8 kuyahama makazi yao kukimbilia katika maeneo salama nchini Sudan na watu milioni 1.2 waliokimbilia nchi jirani kulingana na Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.