Pata taarifa kuu

Sudan: Makundi mawili yenye silaha kutoka Darfur yatangaza kujiunga na jeshi la al-Burhan

Nchini Sudan, nchi iliyo katika vita tangu Aprili 15, 2023, makundi mawili yenye silaha kutoka Darfur yametangaza kujiunga na jeshi la Jenerali al-Burhan. Dhuluma zilizofanywa dhidi ya raia na Vikosi vya Msaada wa Haraka (FSR) magharibi mwa nchi zimeghadhibisha makundi yaSLM-MM na JEM.

Minni Minawi, gavana wa jimbo la Sudan la Darfur, wakati akielekea Port Sudan, Agosti 30, 2023.
Minni Minawi, gavana wa jimbo la Sudan la Darfur, wakati akielekea Port Sudan, Agosti 30, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Nairobi, Gaëlle Laleix

Mnamo Novemba 16, 2023, makundi mawili yenye silaha kutoka Darfur, eneo la magharibi mwa Sudan, yalitangaza kuunga mkono jeshi la Sudan la Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, katika mzozo kati ya wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) wanaoongozwa na Jenerali Mohamed Hamdan Dogolo anayefahamika kwa jina la “Hemedti”. Viongozi wa Vuguvugu la Ukombozi wa Sudan SLM, Minni Minawi, na Vuguvugu la Haki na Usawa (JEM) walitangaza hayo katika mkutano na waandishi wa habari mjini Port Sudan siku ya Alhamisi.

Kufikia sasa, makundi yaliyojihami katika Darfur yalikuwa hayaegemei upande wowote. Lakini unyanyasaji uliofanywa na RSF dhidi ya raia huko Darfur ulikithiri. Katika taarifa ya pamoja, SLM Minni Minawi na JEM wanashutumu "uhalifu dhidi ya binadamu" na "kutangaza ushiriki wao katika operesheni za kijeshi katika nyanja zote".

Kwa Jok Madut Jok, mtafiti katika Chuo Kikuu cha Syracuse nchini Marekani anasema, muungano huu unaweza kubadilisha usawa wa mamlaka ikiwa makundi mengine yatafuata. "Al-Burhan aliongozana naye, katika ziara zake za kidiplomasia, Minni Minawi, kiongozi wa SLM," anaeleza. Hii bila shaka ilituma ujumbe kwa wakaazi wa Darfur ambao hawana asili ya Kiarabu na ambao waliona mauaji ya watu weusi yaliyofanywa na RSF.

Makundi ya waasi huko Darfur yamegawanyika katika makundi mengi. FSR ilitangaza jana, kwenye ukurasa wao ya X, kwamba walifanya mkutano na wanne kati yao. Hali ambayo haijumuishi mkutano wa hadhara, anabainisha naibu kamanda wa Rally of Sudan Liberation Forces, katika gazeti la Sudan Tribune. Anakumbusha kwamba "mapigano huko El Fasher, Kaskazini mwa Darfur, na Al-Dein, Mashariki" ni mstari mwekundu ambao RSF haipaswi kuvuka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.