Pata taarifa kuu

Wanajeshi wa Mali wataka kutumia soka kusherehekea ushindi wa kijeshi wa Kidal

Mamlaka ya Mali inakusudia kuchukua fursa ya mechi mbili za kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2026 la timu ya taifa ya kandanda kusherehekea ushindi wa kijeshi wa hivi majuzi wa jeshi huko Kidal (kaskazini), imesema kwenye mitandao ya kijamii.

Wizara ya Michezo ya Mali "inaalika umma wa wanamichezo na vijana wa Mali kwa uhamasishaji mkubwa (katika hafla ya mechi hizi mbili) kwenye uwanja wa 26-Mars huko Bamako kusherehekea ushindi huu wa kihistoria wa vikosi vya usalama na Eagles ya Mali" wizara hiyo imesema.
Wizara ya Michezo ya Mali "inaalika umma wa wanamichezo na vijana wa Mali kwa uhamasishaji mkubwa (katika hafla ya mechi hizi mbili) kwenye uwanja wa 26-Mars huko Bamako kusherehekea ushindi huu wa kihistoria wa vikosi vya usalama na Eagles ya Mali" wizara hiyo imesema. © GETTY IMAGES
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Michezo inabaini kwenye ukurasa wake wa Facebook kwamba bei ya tikiti kwa wale watakaonunua mwanzo itapunguzwa kwa nusu kwa mechi zilizopangwa Ijumaa huko Bamako dhidi ya Chad, na Jumatatu dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Tikiti hiyo itauzwa kwa faranga 1,000 za CFA (EUR 1.50) badala ya 2,000.

Hii ni "kuruhusu umma wa wanamichezo wa Mali kusherehekea ushindi wa kishujaa wa FAMa (Vikosi vya Jesjhi  la Mali) kwa ushirika na Eagles", jina la utani la wachezaji waliochaguliwa, inasema wizara hiyo.

Jeshi la Mali liliuchukua mji wa Kidal kutoka kwa waasi wa Tuareg siku ya Jumanne, kitovu cha hitaji la uhuru kwa wanaharakati wanaotaka kujitenga ambapo serikali kuu na jeshi Walilifurushwa mwaka wa 2014. Mafanikio haya ya kijeshi, ambayo walipata wanajeshi wa Mali walio madarakani tangu mwaka 2020 katika nchi hii iliyotumbukia katika mgogoro mkubwa wa kiusalama na wa pande nyingi, yalikaribishwa sana na kutoa nafasi kwa maandamano ya furaha kwa mashuja wa kizalendo.

Wizara "inaalika umma wa wanamichezo na vijana wa Mali kwa uhamasishaji mkubwa (katika hafla ya mechi hizi mbili) kwenye uwanja wa 26-Mars huko Bamako kusherehekea ushindi huu wa kihistoria wa vikosi vya usalama na Eagles ya Mali" wizara hiyo imesema.

Shirikisho la kandanda la Mali, katika taarifa kwa vyombo vya habari, limetangaza tu kushuka kwa bei ili "kuruhusu Eagles kuanza vyema" katika kampeni ya kufuzu, bila kutaja ushindi wa Kidal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.