Pata taarifa kuu

Mali: Jeshi lachukua udhibiti wa Kidal, ngome ya waasi wa CSP

Jeshi la Mali limetangaza mnamo Novemba 14, 2023 kuuteka mji wa kimkakati wa Kidal (kaskazini), ngome ya waasi wa CSP. Katika taarifa iliyochapishwa siku ya Jumanne jioni, CSP imekiri kujiondoa kutoka ngome yake ya Kidal, lakini imehakikisha kwamba inaendelea na mapambano dhidi ya serikali kuu.

Muonekano wa angani wa Kidal tarehe 27 Septemba 2020.
Muonekano wa angani wa Kidal tarehe 27 Septemba 2020. AFP - SOULEYMANE AG ANARA
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel

Mashambulio ya Wanajeshi wa Mali (FAMA) kuelekea Kidal yalianza tena Novemba 13, 2023. FAMA na wasaidizi wao wa Urusi walikuwa wamekaribia kilomita kumi na tano kutoka ngome ya waasi wa CSP- PSD.

Siku ya Jumanne asubuhi, FAMA ilitangaza kwamba wanapiga kambi katika eneo hilo. Vyanzo kadhaa vimethibitisha hilo: jeshi la Mali, likiwa na usaidizi mkubwa kutoka kwa mamluki kutoka kampuni ya Kirusi ya Wagner, limepiga kambi katika mji wa Kidal, mji wa kaskazini ulio kuwa chini ya udhibiti wa waasi kwa miaka 11.

Wapiganaji wa mwisho wa waasi wameondoka katika mji wa Kidal. Hii inaimarisha uwepo wa jeshi la Mali na wapiganaji kutoka kampuni ya kijeshi ya Kirusi Wagner katika eneo hilo.

CSP inathibitisha kujiondoa "kwa sababu za kimkakati"

Waasi ambao wengi wao ni kutoka jamii ya Tuareg, wamesema katika taarifa kwamba umejiondoa kutoka Kidal "kwa sababu za kimkakati" baada ya "kwa siku kadhaa kusimamisha jeshi kusonga mbele na hivyo kusababisha hasara kubwa za kibinadamu. "Mapambano yanaendelea," CSP imeongeza.

Huko Kidal, hakukuwa na mapigano kati ya waasi na vikosi vya washirika. Siku ya Jumannejioni, operesheni za usalama zimeendelea. Angalau ndege moja ya jeshi (helikopta) ilitua katika mji huu uliodhibitiwa kwa miaka 11 na waasi walioungana katika muungano uitwao CSP-PSD.

Waasi wa CSP waliondoka eneo hilo na kukimbilia kaskazini kidogo kuelekea Abeïbara, karibu na mpaka na Algeria.

Mbinu sawa ya kupenyeza kama wakati wa kuchukua udhibiti wa Anéfis

Wanajeshi wa Mali na washirika wao waliingia katika mji huo kwa kutumia mbinu ya kupenyeza ambayo tayari ilitumika mwezi mmoja uliopita katika mji ulio kusini zaidi.

Yote yalitokea usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne. Teknolojia kutoka kwa vikosi vya Urusi vinavyosaidia jeshi la Mali ilitumika. Mtaalam anazungumzia "mbinu za kuingilia kwa kutumia miwani ya kuonea usiku". Mbinu hiyo hiyo ilitumiwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita, wakati jeshi la Mali na washirika wake wa Urusi walipochukua udhibiti wa mji wa Anéfis, ulioko kilomita 100 kusini mwa Kidal.

Jiji hili lilikuwa tupu kwa wakaazi wake. Wengi wao walielekea mpaka wa Algeria uliopo kaskazini. Kwa mujibu wa mashahidi wachache tulioweza kuwasiliana nao, hali ya maisha ya raia hao ni ngumu na kama kawaida katika migogoro, wanawake na watoto ndio wengi zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.