Pata taarifa kuu

Mali: Jeshi lakaribia Kidal, mapigano yazuka kilomita chache kutoka mjini

Jeshi la Mali, likisaidiwa na mamluki kutoka kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner, wamezindua vita dhidi ya waasi wa muungano wa CSP-PSD kwa minajili ya udhibiti wa eneo la Kidal Jumamosi hii. Kwa siku kadhaa, mvutano umekuwa ukiongezeka karibu na mji huu wa kimkakati kaskazini mwa Mali.

Msafara wa jeshi la Mali.
Msafara wa jeshi la Mali. AP - Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel

Vita vya Kidal vinaanza. Kwa sasa, mapigano hayo yanaripotiwa katika eneo linaloitwa Alkite, karibu kilomita thelathini kutoka Kidal. Hapa, wanajeshi wa serikali ya Mali, wasaidiwa na mamluki kutoka kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner, wanakabiliana na waasi wa Mali wanaojumuika katika muungano uitwao CSP-PSD.

Kulikuwa na karibu saa mbili za mapigano kwa silaha nzito siku ya Jumamosi, kulingana na mashahidi. Msafara wa jeshi, ambao uliondoka katika mji wa Anéfis saa 24 zilizopita, unaundwa na magari kadhaa.

Lakini pamoja na kupata usaidizi wa ndege za kivita na helikopta, jeshi la Mali halijaweza kuwatimua waasi. Waasi hao wapo uwanjani na wamekatiza mawasiliano rasmi huko Kidal. Hata hivyo, wameshindwa pia kupata ushindi mnono. Kunaripotiwa hasara kubwa katika pande zote ikiwa ni pamoja na vifo kadhaa vya wapiganaji.

Kulingana na habari zetu, mapigano yamesitishwa siku ya Jumamosi jioni na usiku. Jumapili hii pengine itakuwa ya maamuzi kwa matukio mengine, hasa kwa vile pande zote zimeapa kuendelea na mapigano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.