Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

DRC: Machafuko ya kikabila yasababisha vifo vya zaidi ya watu 500 Tshipo

Mapigano yanaendelea kati ya Mbolé na Lenga, jamii mbili katika mkoa wa Tshopo, karibu na mji wa Kisangani, kaskazini-mashariki mwa DRC. Raia sita walifariki wikendi hii, na kufanya idadi ya vifo kufikia zaidi ya 500 tangu mwezi Februari mwaka huu.

Katikati mwa mji wa Kinsagani, DRC.
Katikati mwa mji wa Kinsagani, DRC. Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Hii ni idadi kubwa zaidi ya ile iliyotolewa kwa RFI na vyanzo huru na vya usalama vilivyobaini kwamba watu 250 wameuawa tangu mwezi Februari katika makabiliano kati ya jamii hizo mbili. Mgogoro huu unazidi kutia wasiwasi kwa sababu sasa unakaribia mji wa Kisangani, mji mkuu wa mkoa wa Tshopo.

"Leo kuna takriban siku 5 hadi 6 za utulivu, isipokuwa jana wakati washambuliaji walionekana hadharani. Walijaribu kuwatia wasiwasi wakazi kilomita 184 kutoka mji wa Kisangani. Tangu kuanza kwa mzozo huo mwezi wa Februari, tumerekodi zaidi ya watu 70,000 waliokimbia makazi yao lakini wengi wanapewa hifadhi na familia zao,” anasema Mateus Kanga, msemaji wa gavana wa mkoa wa Tshopo.

“Kinachotisha zaidi ni idadi ya watoto ambao tumeweza kuwasajili. Nyumba kadhaa zimechomwa, hitaji la chakula limeongezeka na kuna wagonjwa... Shida ni kubwa kwa mkoa ambao hauwezi tena kutoa huduma ifaayo,” ameonya msemaji wa gavana wa mkoa wa Tshopo.

Idadi ya waathiriwa imeongezeka katika kipindi cha miezi miwili iliyopita na mamlaka ya mkoa inaonekana kushindwa kukabiliana na mzozo huo, kwani haiwezi tena kuwapa chakula wakimbizi wa ndani kutokana na ukosefu wa uwezo wa kifedha.

Kwa kuhofia hali kuzidi kuwa mbaya, serikali ya kuu imetuma kikosi cha maafisa wa polisi 150 ili kudumisha utulivu katika maeneo yenye mgogoro.

Mgogoro kati ya jamii za Mbole na Lenga umeanza kwa muda wa miezi minane. Mbole nawatuhumu Lenga kwa kuuza ardhi yao kwa kampuni moja kwa miaka 20 ya kazi. Lakini mzozo huo umezidishwa na mauaji na hali ya ulipizaji kisasi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.