Pata taarifa kuu

Mapigano makali yaendelea kati ya M 23 na waasi wa Wazalendo Wilayani Masisi

Mapigano makali yameendelea kushuhudiwa kati ya waasi wa M 23, na wanajeshi wa serikali na makundi mengine ya waasi mwishoni mwa juma hili na kuzua wasiwasi mkubwa Wilayani Masisi jimboni Kivu Kaskazini.

Milima ya Wilaya ya Masisi
Milima ya Wilaya ya Masisi AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Wakaazi wa mji wa Kitshanga wanasema mapigano hayo yamewafikisha waasi wa M 23 kwenye mji huo na sasa wanaudhibiti.

Aidha, wakaazi hao wamesema baadhi ya watu kwenye mji huo wamejeruhiwa katika mapigano hayo na kukimbikizwa hospitalini.

Kwa wiki kadhaa sasa, waasi hao wameendelea kupambana na wale wanaojiita  Wazalendo, wanaodaiwa kuungwa mkono na wanajeshi wa serikali.

Msemaji wa kundi la Wazalendo, ameliambia Shirika la Habari la AFP kuwa mapigano hayo yataendelea, wakati huu yakielezwa kuvuka mpaka na sasa kuingia Wilayani Rutshuru.

Tangu mwezi Oktoba, mji wa Kitshanga umekuwa kwenye doria na vikosi vya Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuepusha mapigano kati ya makundi hayo mawili kabla ya kuondoka na kusababisha mapigano yanayoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.