Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

DRC: Maafisa wa jeshi na polisi wafutwa kazi baada ya kuhusishwa na mauaji ya watu 48 Goma

Serikali ya DRC siku ya Jumatatu ilitangaza kukamatwa kwa maafisa wawili wa kijeshi baada ya vikosi vyao vya jeshi kuhusika katika ukandamizaji dhidi ya maandamano tukio lililosababisha vifo vya watu takriban zaidi ya arobaini siku ya Jumatano ya wiki iliyopita huko Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Maandamano dhidi ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO) huko Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Julai 25, 2022.
Maandamano dhidi ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO) huko Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Julai 25, 2022. © AP Photo/Moses Sawasawa
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka pia imeamua kumuitisha gavana wa kijeshi wa mkoa wa Kivu Kaskazini kwenda Kinshasa "kwa mashauriano", pamoja na "kusimamishwa kazi" kwa maafisa wawili wa polisi, ambao pia wameitishwa katika mji mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani Peter Kazadi alitangaza siku ya Jumatatu jioni mbele ya waandishi wa habari huko Goma.

Waziri Peter Kazadi ni sehemu ya ujumbe rasmi uliofika Goma Jumamosi kutoka Kinshasa "kutoa mwanga" juu ya matukio ya Agosti 30 na "kuweka wazi majukumu ya waliohusika na ghasia hizo", kulingana na maneno ya serikali.

'Tumewahoji wote waliohusika'

Baada ya siku ya kwanza ya mashauriano, Peter Kazadi alitangaza usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu kukamatwa kwa maafisa wawili wa jeshi la Kongo ambao kesi yao, kulingana na chanzo katika ofisi ya mwendesha mashtaka wa kijeshi wa Goma, inaweza kuanza mapema Jumanne au Jumatano.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Wizara ya Mawasiliano ilieleza kuwa maafisa hao ni Kanali Mike Mikombe, Kamanda wa Kikosi cha walinzi wa Jamhuri huko Kivu Kaskazini na Luteni Kanali Donatien Bawili, Kamanda wa kami ya 19 ya Kikosi hicho.

"Tuliwahoji maafisa wote wa usalama wa kijeshi wa jiji hilo," alisema Peter Kazadi, kabla ya kuwaomba "watu wawe watulivu, waiamini serikali na mahakama ambayo itatoa uamuzi wake hivi karibuni."

"Pia tunaomba kila familia ambayo impoteza watu wao, kuripoti kwa afisi ya mwendesha mashtaka mkuu," aliongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.