Pata taarifa kuu

Wachina wawili wameuawa katika shambulio la msafara wa dhahabu DRC

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, raia wawili wa China ni miongoni mwa watu wanne waliouawa na wengine wawili kujeruhiwa, baada ya msafara wao wa magari uliokuwa umebeba dhahabu kushambuliwa na watu wenye silaha, mkoani Kivu Kusini.Β 

Mgodi wa dhahabu katika eneo la uchimbaji madini la Kibali kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Mgodi wa dhahabu katika eneo la uchimbaji madini la Kibali kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Reuters
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea hapo jana wakati msafara wa magari manne, kutoka kampuni ya madini ya TSM yalipokuwa yanasafirisha dhahabu kutoka machimbo ya Kimbi, katika eneo la Fizi.Β 

Mbali na mauaji hayo, imeripotiwa kuwa, wavamizi hao waliiba dhahabu hiyo na kukimbilia msituni, kwa mujibu wa kiongozi wa serikali huko Fizi, Sammy Badibanga Kalondji.Β 

Watu wengine waliouawa ni raia wawili wa DRC, mwanajeshi na dereva, huku waliojeruhiwa wakiwa ni raia mwingine wa China, mwanajeshi wa FARDC na mfanyakazi wa mgodi huo.Β 

Inadaiwa kuwa waliotekeleza mashambulio hayo ni watu wenye silaha, kutoka mkoa jirani wa Maniema.Β 

Nchi ya DRC ina wawekezaji wengi kutoka China waliowekeza kwenye sekta ya madini, lakini pia mkoa wa Kivu Kusini, umeendelea kushuhudia mashambulio yanayolenga maeneo yenye machimbo ya migodi.Β 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.