Pata taarifa kuu

Somalia: Mji wa Baidoa wakabiliwa na vizuizi vya Al Shabab

Nchini Somalia, kundi la wanajihadi la Al Shabab limeweka vizuizi kwa wiki moja kwenye mji wa Baidoa, kusini-magharibi mwa nchi hiyo. Njia nyingi za kuingia au kutoka katika mji huo zimefungwa, kiasi kwamba mkurugenzi mkuu kweye ofisi ya rais wa Somalia amelaani kile alichokiita "vita kamili" dhidi ya raia.

Mji wa Baidoa, Somalia.
Mji wa Baidoa, Somalia. AFP - YASUYOSHI CHIBA
Matangazo ya kibiashara

Hakuna gari, hususan lori, hata punda na trela yake au pikipiki, inayeweza kuingia au kuondoka Baidoa tangu Jumanne Julai 11. Wanamgambo wa Al Shabab wamezuia kila kitu na kuzuia petroli na chakula kufika katika mji huo, ambao hata hivyo unawapa hifadhi wakimbizi wa ndani 600,000 kulingana na Umoja wa Mataifa, na tayari unakabiliwa na athari za ukame na njaa.

Kulingana na vyombo vya habari vya Somalia, bei za vyakula na bidhaa mbalimbali zimepanda na maduka yanaanza kufungwa mji Baidoa. Jumatatu, Julai 17, kampuni ya umeme katika mji huo ilitangaza kwa wateja wake kukatika kwa umeme wakati wa mchana, ili kufidia uhaba wa petroli kwa jenereta zake.

Siku ya Jumapili, Hussein Sheikh Mohamoud, mkurugenzi katika ofisi ya rais wa Somalia, alichapisha ujumbe akisema "anaungana na wakaazi wa Baidoa kwa maumivu walio nayo kufuatia na hali inayowakabili" ya kuwekwa kizuizini bila kutarajia. Alisema kuwa hali hiyo inathibitisha kuwa Al Shabab wanaendesha "vita vya kila namna dhidi ya raia wa Somalia". Kwa upande wake mkurugenzi wa ofisi ya rais wa jimbo ambalo Baidoa inapatikana, Abdifatah Mahat, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba Al Shabab tayari walikuwa wameweka vizuizi katika miji ya jimbo jirani la Hiraan, na kwamba utumiaji nguvu ndio pekee uliyoviondoa. 

Serikali ya Somalia, kwa upande wake, inasema inajiandaa kuanzisha operesheni inayoitwa "Black Lion" (Simba Mweusi), hasa karibu na Baidoa, awamu ya pili ya kampeni yake ya kijeshi ya kitaifa dhidi ya wanajihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.