Pata taarifa kuu
SIASA-UCHAGUZI

Aige: Wananchi wa Mali wameidhinisha rasimu ya katiba mpya kwa asilimia 97 ya kura

Nchini Mali, kura ya 'Ndiyo' imeshinda kwa 97%, kulingana na Mamlaka Huru ya Kusimamia Uchaguzi (Aige) iliyotangaza siku ya Ijumaa jioni, matokeo ya kura ya maoni iliyofanyika Jumapili Juni 18, 2023, kuhusu rasimu ya Katiba Mpya inayotafutwa na mamlaka ya mpito ya Mali.

Afisa wa uchaguzi akiangalia nyaraka katika kituo cha kupigia kura huko Bamako mnamo Juni 18, 2023, kabla ya kura ya maoni nchini Mali.
Afisa wa uchaguzi akiangalia nyaraka katika kituo cha kupigia kura huko Bamako mnamo Juni 18, 2023, kabla ya kura ya maoni nchini Mali. AFP - OUSMANE MAKAVELI
Matangazo ya kibiashara

97% ya kura ya 'Ndio', dhidi ya 3% kura ya 'Hapana'. Ni ushindi wa kishindo, kama unavyoweza kutarajia. Waliohamasishwa ni wafuasi wa mamlaka ya mpito na rasimu yao ya Katiba mpya. Wale walioupinga walipendelea kususia uchaguzi huo, kwani vyama vingi vya upinzani viliwataka kufanya hivyo. Tunachoweza kukumbusha ni kiwango cha ushiriki cha 39.40%, karibu 40%. Hiki ni kiwango cha juu sana. Waangalizi wa uchaguzi walibaini kwa upande wao kwamba waliojitokeza katika kura hiyo ya maoni walifikia  28%. Alama 12 zimezidi.

Somo jingine kutoka kwa takwimu zilizotangazwa na Mamlaka Huru ya Kusimamia Uchaguzi (Aige) jioni ya leo. Wanajeshi, ambao walipiga kura ya mapema mnamo Juni 11, wiki moja kabla ya watu wengine, walishiriki kwa zaidi ya 73%. Na walipiga kura ya 'Ndiyo' kwa karibu 94%. Idadi hiyo ni kubwa, lakini ni chini ya idadi ya watu wengine, ambayo inaweza kuonekana kuwa ya kushangaza.

Mabishano kuhusu kura katika jimbo la Kidal

Aige imebainisha kuwa matokeo yatatolewa ofisi kwa ofisi kwenye tovuti yake. Wasiwasi huu wa uwazi, ambao haujafikia hatua ya kujibu shutuma nyingi za udanganyifu zilizotolewa siku za hivi karibuni na vyama vya siasa au mashirika ya kiraia, ambayo yametaja kujaza masanduku ya kura au hata kura za uwongo katika maeneo ambayo raia wametoroka makazi yao kutokana na machafuko ya wanajihadi.

Pia hakuna maelezo kuhusiana na utata uliojitokeza kuhusu kura ya maoni katika jimbo la Kidal. Waangalizi wa uchaguzi kwa kauli moja wanahakikisha kwamba kura hiyo haiwezi kufanyika popote katika eneo hilo, jambo ambalo pia lilithibitishwa na makundi yenye silaha yaliyotia saini makubaliano ya amani, ambayo yanadhibiti sehemu hii ya eneo hilo. Hata hivyo Aigeimetangaza kwamba kura ya maoni ilifanyika "nchini kote". Hatu inayofuata ni Mahakama ya Katiba kuidhiniha au la matokeo hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.