Pata taarifa kuu

Mali: Makundi ya waasi yaonya kuhusu hatua ya MINUSMA kuondoka

Nairobi – Ikiwa wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa Mataifa, wataondoka nchini Mali, itakuwa pigo kwa mkataba wa amani na kutishia ustawi wa taifa hilo na ukanda, hii ni kauli ya muungano wa makundi ya waasi kaskazini mwa nchi hiyo.

Wanajeshi wa umoja wa mataifa wa kulinda amani nchini Mali, MINUSMA
Wanajeshi wa umoja wa mataifa wa kulinda amani nchini Mali, MINUSMA © Souleymane Ag Anara / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Makundi hayo imekuja siku chache baada ya Serikali kukitaka kikosi hicho cha kulinda amani, Minusma kuondoka bila kuchelewa, matakwa ambayo yalifuatia miaka mingi ya kuvunjika kwa uhusiano kati ya Umoja wa Mataifa na uongozi wa kijeshi wa Bamako.

kiongozi wa kijeshi Assimi Goita anaushutumu ujumbe huo kuwa sio tu umeshindwa kulinda amani, bali pia umekuwa sehemu ya tatizo lililopo nchini humo na hivyo kuongeza vizuizi dhidi ya operesheni za walinda Amani katika maeneo kadhaa hususan kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa upande wake mkuu wa jeshi la MINUSMA, El Ghassim Wane amesema kikosi cha wanajeshi wa umoja wa mataifa kinatarajiwa kumaliza operesheni zake hadi Juni 30 mwaka huu.

Ifahamike kuwa Utawala wa Mali tayari umekatisha ushirikiano wa muda mrefu na Ufaransa na washirika wengine wa Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.