Pata taarifa kuu

Cameroon: John Fru Ndi, mpinzani wa kihistoria wa Rais Paul Biya aaga dunia

Mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji wa kihistoria wa Rais Paul Biya wa Cameroon, John Fru Ndi, aliadhimisha "miaka ya makaa" mwanzoni mwa miaka ya 1990, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.

Kiongozi wa Chama cha Social Democratic Front (SDF) cha Cameroon, John Fru Ndi, akiwasili kuhutubia kongamano la chama chake mjini Bamenda Februari 22, 2018.
Kiongozi wa Chama cha Social Democratic Front (SDF) cha Cameroon, John Fru Ndi, akiwasili kuhutubia kongamano la chama chake mjini Bamenda Februari 22, 2018. AFP - REINNIER KAZE
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa Social Democratic Front (SDF) amefariki akiwa na umri wa miaka 81, kimetangaza chama chake cha SDF. Mkutano wa chama chake, mnamo Julai 28, 29 na 30, 2023, ungelizingatia uamuzi wa kumuondoa katika maisha ya kisiasa.

Mchuuzi huyu wa vitabu anayezungumza Kiingereza alidhihirisha, katika miaka ya 1990, upinzani mkali kwa Rais Paul Biya. John Fru Ndi alizaliwa mwaka wa 1941 huko Baba II, kijiji cha Mezam, karibu na Bamenda, katika eneo ambalo sasa ni Kaskazini Magharibi, ambalo wakati huo lilikuwa Kaskazini mwa ameroo, eneo linalosimamiwa na Uingereza chini ya mamlaka ya Umoja wa Mataifa.

Baada ya kuondoka kwenda kusoma nchini Nigeria, alirudi Bamenda ambako alifanya kazi kadhaa, ikiwa ni pamoja na ya uuzaji wa vitabu. Mwishoni mwa miaka ya 1980, aljiunga na watu wengine kupitia orodha ya CPDM, wakati huo kikiwa chama kimoja.

Alikuwa na umri wa karibu miaka 50 aliposhiriki katika uundaji wa chama cha Social Democratic Front (SDF). Chama hiki sio chaguo la kwanza, lakini alikubali kuchukua uonozi wa chama hiki, licha ya hatari. Mnamo Mei 26, 1990, huko Bamenda, mkutano wa kuanzishwa kwa chama kipya ulikandamizwa kwa umwagaji damu.

John Fru Ndi alionyesha taswira ya kiongozi shupavu asiyerudi nyuma. Umaarufu wake unakwenda mbali, zaidi ya mikoa inayozungumza Kiingereza. Alikuwa maarufu katika mikoa ya Magharibi na Littoral ambapo mji mkuu wa kiuchumi wa Douala unapatikana.

Mshindi wa pili katika uchaguzi wa rais wa 1992

Katika miaka ya 1990 na 1991, iliyoangaziwa na vuguvugu la kususia shughuli za serikali, hadi uchaguzi wa urais wa vyama vingi mnamo 1992, aliwakilisha matumaini kwa wale waliotaka mabadiliko karibu na kauli mbiu "Biya lazima aende / Biya lazima aondoke".

John Fru Ndi ambaye alitangazwa kushindwa uchaguzi wa urais, alipinga takwimu rasmi ambazo zilimpa nafasi ya pili. Alisusia uchaguzi wa urais wa mwaka 1997, akagombea tena dhidi ya Paul Biya mwaka wa 2004. Kisha, tena, mwaka wa 2011, kampeni yake ya mwisho.

John Fru Ndi ameedelea kuwa mkuu wa chama chake kwa miaka thelathini na tatu, hadi kifo chake. Anakufa bila kujua mabadiliko ambayo alitamani kuwa mkuu wa nchi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.