Pata taarifa kuu
UCHANGANUZI-USALAMA

Cameroon: Makundi yenye silaha yabadili mkakati katika vita vyao

Baada ya kushindwa katika vita, kutokana na kudhoofika na kugawanyika kwao, wanaharakati walioshika silaha kwa kutaka maeneo yao kuwa huru 'Ambaboys' wamebadili njia mpya katika mapambano yao, wanajihusisha kwa sasa na tekaji nyara na kutaka fidia kwa mateka wanaoshikilia, lakini pia mashambulizi. Wanafanya hivyo ili kuonyesha uhalali wao kwa wananchi.

Wanawake hupita kando ya soko lililotelekezwa kwa moto huko Buea, katika mkoa wa Kusini Magharibi ambao watu wengi huzungumza Kiingereza, Oktoba 3, 2018, karibu na mabaki ya gari linalodaiwa kuchomwa moto na wapiganaji wanaotaka kujitenga katika shambulio la hivi majuzi.
Wanawake hupita kando ya soko lililotelekezwa kwa moto huko Buea, katika mkoa wa Kusini Magharibi ambao watu wengi huzungumza Kiingereza, Oktoba 3, 2018, karibu na mabaki ya gari linalodaiwa kuchomwa moto na wapiganaji wanaotaka kujitenga katika shambulio la hivi majuzi. AFP - MARCO LONGARI
Matangazo ya kibiashara

Je, ni urekebishaji mpya, katika muda, wa mfumo wa vitendo vya makundi ya watu wanataka kuojitenga wenye silaha, katika maeneo yanayozungumza Kiingereza ya Kaskazini-Magharibi na Kusini-Magharibi, nchini Cameroon? Tukio la hivi majuzi limeweka swali hili mezani.

Mnamo Mei 19, 2023, katika eneo la Kedjom Keku, sio mbali na Bamenda, mji mkuu wa mkoa wa Kaskazini-Magharibi, wanawake thelathini walifanya maandamano ya amani, kulingana na vyanzo rasmi, kupinga vitendo vya makundi ya kupigania uhuru ambayo vinalazimisha raia kulipa "kodi" kwa manufaa yao.

Siku iliyofuata, waandamanaji hao walitekwa nyara na wapiganaji wa makundi hayo, kabla ya kuachiliwa siku nne baadaye. Kulingana na mamlaka katika maeneo hayo, wanawake hao thelathini waliteswa wakati wa kuzuiliwa kwao. Habari hii haiiungwi mkono na wote. Kulingana na mchambuzi aliyefahamishwa kuhusu masuala ya usalama katika eneo hilo, aliyehojiwa na RFI, “wanawake haw hawakunyanyaswa kwa sababu kwa hakika kulikuwa na urushianaji risasi kati ya wanajeshi wa serikali na waasi hao. Hivi ndivyo makundi haya sasa yanaishi, au hasa zaidi majambazi hawa wanaotumia vita kama uchumi sasa, baada ya makundi [ya silaha] kuvunjwa na kusambaratishwa na vikosi vya serikali. "

“Wamedhoofishwa sana na migogoro ya ndani kati ya makundi mbalimbali. Hawaendeshi shughuli zao tena katika maeneo ya mijini, ambako hata hivyo wanabakisha wanachama kadhaa, na wamekimbilia vijijini. Hapa ndipo wanaponyanyasa watu, kutekeleza utekaji nyara, na kuwanyang’anya pesa,” anasema Yerima Kini Nsom, mhariri mkuu wa Gazeti la The Post, gazeti linaloheshimika kwa lugha ya Kiingereza kila baada ya wiki mbili, ambalo linafuatilia kwa karibu mgogoro huo tangu kuzuka kwake mwishoni mwa mwaka 2016.

Uhalali mashakani

Hata kama wamedhoofika, "Ambaboys" pia wanaendelea kuhangaisha vikosi vya usalama. “Tunaona wazi kwamba makundi haya, au wale wanaodai kuwa wa kwao, wanafanya mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa serikali au vituo vya polisi au kwenye barabara kuu ya umma, wanavizia vikosi vya ulinzi na mamlaka, kushambulia misafara yao. Upekee wa vitendo hivi upo katika matumizi ya mabomu ya ardhini na vifaa vya vilipuzi vilivyoboreshwa. Hatuwezi kusahau vizuizi walivyoweka katika baadhi ya maeneo", anasema mwanahistoria na mtaalamu wa mambo ya baadaye Raoul Sumo Tayo, katika Kitivo cha Sayansi ya Jamii cha Chuo Kikuu cha Louvain, na mtafiti katika Kituo cha Mafunzo na Utafiti katika Amani, Usalama na Utangamano wa Chuo Kikuu cha Maroua (Cameroon).

Je, 'Ambaboys' watafikia wapi katika mchakato wao mpya kwa vita vyao vya kupigania uhuru wa maeneo yao yanayozungumza Kiingereza?

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.