Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Wanawake thelathini watekwa nyara magharibi mwa Cameroon

Waasi wanaotetea uhuru wa maeneo yao wanawashikilia wanawake "takriban thelathini" ambao walikuwa wakiandamana kupinga unyanyasaji unaowakabili magharibi mwa Cameroon, eneo la vita vikali kwa zaidi ya miaka sita kati ya watu wanaotaka kujitenga kutoka jamii ya watu wachache wanaozungumza Kiingereza na polisi, mamlaka imesema siku ya Jumanne.

Siku iliyotangulia, wanawake hawa "wazee" walipanga "maandamano ya amani kupinga (...) dhidi ya visa vya magaidi na uhalifu", Halmashauri ya wilaya ya Mezam imeongeza.
Siku iliyotangulia, wanawake hawa "wazee" walipanga "maandamano ya amani kupinga (...) dhidi ya visa vya magaidi na uhalifu", Halmashauri ya wilaya ya Mezam imeongeza. © Marco Longari, AFP
Matangazo ya kibiashara

"Wanawake hao waliteswa vikali na kutekwa nyara na magaidi waliokuwa na silaha" katika kijiji cha Kedjom Keku, katika jimbo la Kaskazini Magharibi, ambako makundi yenye silaha yanayotaka kujitenga mara kwa mara huwateka nyara raia, hasa kwa ajili ya fidia, halmashauri ya wilaya ya Mezam imesema katika taarifa iliyotolewa Jumanne Mei 23. 

Siku iliyotangulia, wanawake hawa "wazee" walipanga "maandamano ya amani kupinga (...) dhidi ya visa vya magaidi na uhalifu", Halmashauri ya wilaya ya Mezam imeongeza. 

Mamlaka bado inatumia neno "magaidi" kubaini waasi wenye silaha ambao wanadai uhuru wa mikoa ya Kaskazini Magharibi na Kusini Magharibi, inayokaliwa zaidi na watu wachache wanaozungumza Kiingereza katika nchi hii ya Afrika ya Kati yenye watu wengi wanaozungumza Kifaransa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.