Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-SIASA

Senegal: Mazungumzo ya kitaifa kuzinduliwa katika mazingira ya mivutano ya kisiasa

Rais Macky Sall ataanzisha Jumatano hii, "mazungumzo ya kitaifa", miezi tisa kabla ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi Februari 2024. Rais Macky Sall bado hajasuluhisha mjadala wa uwezekano wa kugombea muhula wa tatu. Sehemu ya upinzani tayari imekataa kushiriki mazungumzo hayo, na unakusudia kuandaa mazungumzo yake. Juhudi katika mazingira ya mvutano wa kisiasa, huku hukumu katika kesi ya mpinzani Ousmane Sonko kwa mashtaka ya ubakaji ikitarajiwa kutolewa siku ya Alhamisi.

Macky Sall, Rais wa Jamhuri ya Senegal, anatarajiwa kuzindua mazungumzo ya kitaifa Jumatano hii.
Macky Sall, Rais wa Jamhuri ya Senegal, anatarajiwa kuzindua mazungumzo ya kitaifa Jumatano hii. © Présidence sénégalaise
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Dakar, Charlotte Idrac

Mkutano huo umepangwa saa kumi jioni katika ukumbi wa karamu ya ikulu ya rais kwa hafla ya uzinduzi rasmi. Hapo awali mkutano huo ulipangwa kufanyika siku ya Jumanne, uliahirishwa kwa saa 24 bila maelezo kutoka kwa mamlaka. "Mazungumzo ni mila nchini Senegal" amesema msemaji wa serikali, "maswali yote yatajadiliwa".

Baada ya "mashauriano", chama cha Taxawu Senegal cha Khalifa Sall kimethibitisha uamuzi wake wa kushiriki. Kushiriki "kwa uwajibikaji, lakini bila kuathiri mapamano yanayofanywa katika upinzani" imebaini taarifa yake kwa vyombo vya habari. Chama hicho kinasema kiko "kwenye mstari wa mbele" dhidi ya "Macky Sall kugombea muhula wa tatu kinyume na katiba".

Baada ya kuhukumiwa, mgombea urais aliyetangazwa Khalifa Sall hana haki ya kuwania katika uchaguzi huo kwa wakati huu. Kama vile Karim Wade, mtoto wa rais wa zamani. Chama chake, PDS, kilikuwa tayari kimekubali kimsingi kushiriki katika mazungumzo hayo. Suala kuu kwao litakuwa marekebisho ya kanuni za uchaguzi au msamaha ili kuwaruhusu kushindana.

Lakini kwa viongozi wengine wengi wa upinzani - Ousmane Sonko, Déthié Fall au hata Aminata Touré - hakuna suala la kushiriki katika kile wanachokiita "mkataba". Wanatoa wito wa kujiunga na "mazungumzo ya raia" yaliyoandaliwa na jukwaa la F24 Jumatano hii alasiri. Miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa: "kutojaribu tena kugombea kwa muhula wa 3" na "kugawana vizuri madaraka".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.