Pata taarifa kuu

Senegal: Makabiliano yazuka karibu na nyumba ya Ousmane Sonko

Nchini Senegal, makabiliano yalizuka, Jumatatu hii, Mei 29, kati ya waandamanaji vijana na maafisa wa polisi mjini Dakar, hasa karibu na nyumba ya Ousmane Sonko. Mtaa wake ulikuwa umezingirwa.

Mtu huyu akijaribu kuzima moto wakati wa maandamano huko Dakar mnamo Mei 29, 2023 kupinga kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko.
Mtu huyu akijaribu kuzima moto wakati wa maandamano huko Dakar mnamo Mei 29, 2023 kupinga kukamatwa kwa kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Dakar, Charlotte Idrac

Jumatatu hii jioni, matairi yaliyochomwa kwenye mhimili wa barabara unaoitwa "VDN". Katika viunga vya wilaya ya Cité Keur Gorgui, maafisa wa polisi walizuia mkusanyiko wowote katika mtaa huo na vizuizi vimewekwa ili kufunga barabara anakoishi Ousmane Sonko.

Mbele kidogo, makundi madogo ya vijana yamekuwa yanajaribu kukaribia kwenye makaazi ya Ousmane Sonko, huku yakirusha mawe… Polisi walijibu kwa mabomu ya machozi.

Kiongozi huyo wa upinzani, ambaye alikuwa ametoa tangazo Jumapili jioni, bado hajazungumza hadharani. Kulingana na meneja wa mawasiliano wa chama cha Pastef cha Ousmane Sonko, timu ya kiufundi ilikataliwa kuingia nyumbani kwake, kama vile wabunge wa upinzani na wanachama wa jukwaa la F24 ambao walitaka kumtembelea. Msafara wa Ousmane Sonko unashutumu "uhalisia na kizuizi cha nyumbani kinyume cha sheria".

Kwa upande wake, serikali ilisisitiza siku moja baada ya kesi ya mpinzani ya "kudumisha utulivu wa umma", "kipaumbele", kulingana na msemaji wake. Senegal ni "nchi yenye sheria", amebainisha Waziri wa Mambo ya Ndani.

"Kwa sababu za kiusalama", gavana wa Dakar kwa mara nyingine tena amepiga marufuku pikipiki kutembea katika mji huo hadi Jumanne, Mei 30 saa kumi na moja jioni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.