Pata taarifa kuu
HAKI-SIASA

Senegal: Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko akabiliwa na kifungo cha miaka kumi kwa ubakaji

Nchini Senegal, macho yote yalikuwa yakitazama hadi usiku wa manane kuelekea mahakama ya Dakar ambako kesi ya kiongozi wa upinzani wa kisiasa Ousmane Sonko ilikuwa ikiendelea, licha ya kuwa hakuripoti mahakamani, akifunguliwa mashitaka ya ubakaji na mfanyakazi wa zamani wa chumba cha masaji. 

Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko, mjini Ziguinchor mnamo Julai 3, 2022.
Kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko, mjini Ziguinchor mnamo Julai 3, 2022. AFP - MUHAMADOU BITTAYE
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Ousmane Sonko, ambaye ni mgombea urais katika  uchaguzi wa urais wa mwaka 2024 ananalaani njama ya kumuondoa kwenye mchezo wa kisiasa. Muda kidogo baada ya saa tatu asubuhi, Mei 24, mwendesha mashtaka aliomba dhidi yake miaka 10 jela kwa ubakaji au miaka 5 kwa ufisadi wa ujana. Mahakama inatarajia kutoa uamuzi wake tarehe 1 Juni mwaka huu.

Wakili El Hadj Diouf, mwanasheria wa Adji Sarr, alimshutumu Ousmane Sonko kwa kutaka "kukimbia haki": "Nchi yetu, Senegal, leo ndiyo kwanza imefanya kesi muhimu kwa mustakabali wake, kwa uthabiti wake na huyo ni Sonko mwenyewe ambaye alisema alikuwa na haraka ya kwenda kusisikiliza hukumu! Anaogopa nini? Ukwelu mtupu! Lakini licha ya yote,kesi hiyo ilisikilizwa. Sijaridhika kabisa na mashtaka ya upande wa mashtaka. Sasa, ili kuendeleza vizuri hoja zinazotetea kuhukumiwa kwa ubakaji. Ikiwa ofisi ya Mashtaka ya Umma itakuja, jaribu kukata peari kwa nusu kwa kusema: ikiwa haujashawishika na ubakaji, uhifadhi ufisadi wa vijana, hapana, hiyo haionekani kwangu kuwa kali. "

Njama za kisiasa?

Baada ya kupitishwa kwa mashahidi kati ya nane mchana na usiku wa manane, mawakili wa Adji Sarr waliendelea na maombi yao. Kiini cha mijadala: cheti cha matibabu na ubikira wa Adji Sarr, uwepo wa manii kwenye sehemu yake ya siri au siku aliyowasilisha malalamiko.

Kinyume chake, mawakili wa Ousmane Sonko, ambao wanashutumu njama ya kisiasa, hawakuweza kujibu bila kuwepo kwa mteja wao. Mtuhumiwa mkuu na kiongozi wa upinzani nchini Senegal amejikita katika ngome yake ya Ziguinchor kwa muda wa wiki mbili. Mawakili wake waliondoka kwenye chumba hicho saa sita mchana, anakumbusha Charlotte Idrac, mwandishi wetu wa habari huko Dakar. Wanadai kuwa mpinzani hakuwa amepokea wito unaofaa. wakili Ousseynou Ngom anashutumu "ukiukwaji wa haki za utetezi": "Lazima iwe wazi, Ousmane Sonko hakukataa kutokea, Ousmane Sonko aliomba haki zake ziheshimiwe, hasa kwamba aitwe mara kwa mara, kwa mujibu wa sheria, ambayo haijafanywa. Kwa hivyo chini ya masharti haya, ni wazi, tuliomba kufukuzwa kwa kuhalalisha hali yake, na hakimu alikataa tena, na akahifadhi kesi hiyo. Tunakemea, tumekasirishwa kuhusiana na ukiukaji huu wa haki. Lengo linalotafutwa ni kumzuia Ousmane Sonko asionekane na kuwa na uamuzi bila kuwepo. "

Kulingana na kanuni za uchaguzi, "mtu ambaye hayupo" hawezi kusajiliwa kwenye orodha za wapiga kura: kwa hivyo ni kustahiki kwa Ousmane Sonko kwa uchaguzi wa urais wa 2024 ambao uko hatarini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.