Pata taarifa kuu

Senegal : Sonko akosa kufika mahakamani kwa mara nyengine

NAIROBI – Nchini Senegal, kiongozi wa upinzani Ousmane Sonko aliyeshtakiwa kwa madai ya ubakaji, kwa mara ya pili leo, ameshindwa kufika Mahakamani, kusikiliza kesi inayomkabili. 

Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko
Kiongozi wa upinzani nchini Senegal Ousmane Sonko © AFP - Seyllou
Matangazo ya kibiashara

Kuanzia mapema leo Jumanne, polisi jijini Dakar waliimarisha usalama ndani na nje ya Mahakama kwa hofu kuwa ya kutokea kwa fujo kutoka kwa wafuasi wa kiongozi huyo wa upinzani. 

Awali, mwanasiasa huyo alikuwa amedokeza kuwa, asingefika Mahakamani iwapo usalama usingehakikishiwa na vyombo vya ulinzi na usalama. 

Hata hivyo, hali ya utulivu imeshuhudiwa kinyume na hali ilivyokuwa siku kadhaa zilizopita, ambapo wafuasi wa Sonko walikabiliana na polisi. 

Sonko, ambaye ana ushawishi mkubwa hasa kwa vijana, anaishtumu serikali kwa kutumia siasa na kutumia kesi hiyo ili kumzuia asiwanie urais mwaka ujao. 

Mwanasiasa huyo wa upinzani, ameshtakiwa kwa madai ya ubakaji na kumtishia kumuua, mfanyakazi wa duka la urembo madai amabyo ameyakanusha. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.