Pata taarifa kuu

CAR: Serikali yatoa wito wa uvumilivu baada ya kisa cha moto katika kiwanda cha Castel

Baada ya kisa cha moto ulioteketeza sehemu ya ghala la kampuni ya bia ya Mocaf, kampuni tanzu ya kundi la Ufaransa la Castel huko Bangui nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, usiku wa Jumapili Machi 5 kuamkia Jumatatu Machi 6, vyanzo vinahusisha wapiganaji wa kundi la kijeshi la Kirusi Wagner katika kitendo hiki cha uhalifu. Lakini serikali inatoa wito wa uvumilivu wakati ikisubiri matokeo ya uchunguzi wa wazi.

Picha ya pili ya CCTV ya moto ulioteketeza sehemu ya ghala la kampuni ya pombe ya MOCAF, kampuni tanzu ya kundi la Ufaransa la Castel mjini Bangui.
Picha ya pili ya CCTV ya moto ulioteketeza sehemu ya ghala la kampuni ya pombe ya MOCAF, kampuni tanzu ya kundi la Ufaransa la Castel mjini Bangui. © Capture d'écran vidéo surveillance
Matangazo ya kibiashara

Usiku wa Jumapili Machi 5 kuamkia Jumatatu Machi 6, karibu "saa saba usiku", moto, mbaya kwa mujibu wa serikali, ulizuka baada ya kurusha vifaa vibaya vilivyoteketeza vifaa vya kiwanda cha bia cha Mocaf (kifupi Motte Cordonnier Afrique) huko Bangui.

Vyanzo vilivyohijiwa na RFI vinawahusisha wapiganaji wa kundi la wanamgambo wa Urusi Wagner katika kitendo hiki, baada ya kutazama video zilizorekodiwa siku hiyo ya tukio.

Akihojiwa na Esdras Ndikumana, kutoka kitengo cha RFI ukanda wa Afrika, msemaji wa Ikulu ya rais, Albert Yloké Mokpemé anatoa wito wa uvumilivu wakati wa kusubiri matokeo ya uchunguzi unaoendelea, huku akiwashambulia wale ambao walikuwa na nia, anasema, kulaani "Warusi" vibaya.

Mvua ikinyesha leo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wanasema ni Warusi. Kunapokuwa na joto sana, baadhi - na hasa nchi za Magharibi - vyombo vya habari husema ni Warusi. Niwaambie tu kwamba leo tuna washirika ambao ni wakufunzi wa Kirusi na vikosi vyetu vya ulinzi na usalama, ambao wanalinda usalama wa nchi hii kwa mafanikio makubwa. Haifurahishi wanaotaka ukosefu wa usalama, wanaotaka kuyumbisha nchi yetu.
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.