Pata taarifa kuu

Je, Marekani na CAR zinajadili kuhusu kuondoka kwa mamluki wa Wagner?

Hii ni habari ambayo imekuwa ikisambaa hivi karibuni katika vyombo vya habari vya kimataifa, ambavyo vimepata nyaraka za ndani za Marekani.

Wapiganaji wa Wagner katika makao makuu ya St. Petersburg yalifunguliwa mnamo Novemba 2022.
Wapiganaji wa Wagner katika makao makuu ya St. Petersburg yalifunguliwa mnamo Novemba 2022. AP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyombo vya habari hivi, Washington itajitolea kwa mamlaka ya Afrika ya Kati kutoa mafunzo kwa jeshi lake na kuongeza misaada yake ya kibinadamu kwa kubadilishana na kutimuliwa kwa wanajeshi wa Wagner nchini humo. Washington inasemekana kutoa pendekezo hili - katika mfumo wa makubaliano - kwa Rais Touadéra wakati wa mkutano wa kilele wa Marekani na Afrika mwezi Desemba mwaka janahuko Washington, kulingana na gazeti la Ufaransa, Le Monde.

Habari hii ilikanushwa katika siku za hivi karibuni. Kwa upande wa serikali ya Bangui, hii ni habari ya uwongo. "Watu wanazungumza mengi kuhusu wasichokijua," amejibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika ya Kati, Sylvie Baïpo-Temon. Anakiri, hata hivyo, kwamba kuna majadiliano yaliyofanyika na Marekani, kuhusu ushirikiano ulioimarishwa, akiongeza kuwa kwa kufanya kazi kwa ukarimu, na kwa muda, na Marekani, ambapo pia alizuru mara kadhaa katika miezi ya hivi karibuni.

"Sijapata waraka huo" amejibu msemaji wa ofisi ya rais, Albert Yaloke Mokpeme, ambaye anaona kama kampeni chafu dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. Anakumbusha kwamba balozi wa Marekani huko Bangui mwenyewe alikanusha taarifa hizo.

Marekani "inaheshimu uhuru wa Jamhuri ya Afrika ya Kati," Ubalozi wa Marekani umeandika kwenye mitandao ya kijamii, na kuongeza kuwa onyo kutoka nchi hiyo ya Jamhuri y Afrika ya Kati na kufungwa kwa Ubalozi wa Marekani ni uongo.

Habari za kweli au za uwongo, mabishano hayo yanakuja huku Marekani ikijaribu kuzuia ongezeko la kundi la wanamgambo wa Urusi katika barani Afrika. Na kupitisha vikwazo vipya dhidi ya kundi hili la mamluki wa Urusi la Wagner, ikiwa ni pamoja na kuzuia mali yoyote ambayo kundi la wanamgambo hao wanaweza kuwa nayo nchini Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.