Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Waasi wa M23 nchini DRC: Mapigano yarindima, licha ya mkutano mpya

Mapigano yamepamba moto Jumatatu kati ya jeshi na waasi wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, siku tatu baada ya mkutano mpya wa wa viongozi wa Umoja wa Afrika na ule wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo wakaazi wa eneo hilo wanasema hawana matumaini yoyote.

Mwanajeshi wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC).
Mwanajeshi wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (FARDC). AFP PHOTO/PHIL MOORE
Matangazo ya kibiashara

"Kumekuwa na mapigano tangu saa 5:00 asubuhi kati ya jeshi la DRC, FARDC, na M23", katika eneo la Kitshanga kuelekea Mweso, huko Masisi, takriban kilomita mia moja kaskazini magharibi mwa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini, kimebaini chanzo cha usalama ambacho hakikutaka kutotajwa jina.

Kwa mujibu wa Toby Kahangu, afisa wa shirika la kiraia katika eneo hilo, M23 ilikuwa Jumatatu katika eneo la Muhongozi, takriban kilomita 3 kutoka Mweso, mtaa uliopo kwenye moja ya barabara kuu za Masisi, eneo lenye rutuba kwa utajiri wa madini.

"Ni waasi, hawajali mikutano ya Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Afrika Mashariki," afisa huyu amesema, akimaanisha mikutano iliyofanyika mwishoni mwa juma mjini Addis Ababa.

Kabla ya mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika (AU), wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), waliokutana Ijumaa, walitoa wito tena wa "kusitishwa mara moja kwa mapigano" na kutaka "makundi yote yenye silaha kuondoka katika maeneo wanaoshikilia ifikapo Machi 30" mashariki mwa DRC.

"Katika mikutano yote iliyofanyika, huko Luanda, Nairobi au Bujumbura, maazimio huchukuliwa na kamwe hayatumiki", pia anasema, akiwa amekata tamaa, Gentil Sonny Mulume, mwanaharakati wa vuguvugu la kiraia Lucha (mapambano kwa ajili ya mabadiliko). "Hatuoni mwanga wa matumaini... Wanaendelea kuwavuruga raia wa Kongo na kumlaghai mkuu wa nchi" Félix Tshisekedi, anaongeza.

Kundi la M23, la "Movement of March 23", ni waasi ambao wengi wao nikutoka jamii ya Watutsi ambao walichukua silaha tena mwishoni mwa mwaka 2021, wakiishutumu Kinshasa kwa kutokuwa na ahadi zinazoheshimiwa za kuwarejesha wapiganaji wake katika maisa ya kiraia na wengine kuwaunganisha na vikosi vya usalama na jeshi. Tangu wakati huo imeteka maeneo makubwa ya kaskazini na kaskazini-magharibi mwa Goma.

Kinshasa inaishutumu Rwanda kwa kuunga mkono uasi huu, madai ambayo ynathibitishwa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa na nchi kadhaa za Magharibi, ingawa Kigali inakanusha. Juhudi kadhaa za kidiplomasia, ambazo hazijafanikiwa hadi sasa, zimeanzishwa, hususan na EAC, ambayo imeunda kikosi cha kikanda kinachopaswa kuhakikisha kuwaondoa M23 kwenye maeeo wanayoshikilia kwa mwaka mmoja.

Kama vile ujumbe wa Umoja wa Mataifa, unaoshutumiwa kwa kushindwa kukabiliana na makundi mengi yenye silaha ambayo yamekuwa yakishambulia mashariki mwa DRC kwa karibu miaka 30, kikosi hiki cha kikanda kinazidi kukosolewa na wakazi wa mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.