Pata taarifa kuu
HAKI-SHERIA

Amnesty: Makumi ya wanawake walibakwa na waasi wa M23

Makumi ya wanawake walibakwa na waasi wa M23 katika mfululizo wa mashambulizi kati ya Novemba 21 na 30 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International limesema leo Ijumaa.

Wapigaanji wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mnamo Januari, 2023.
Wapigaanji wa M23 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mnamo Januari, 2023. AFP - GUERCHOM NDEBO
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na ushuhuda wa waathiriwa 35 na mashahidi wa moja kwa moja, shirika la haki za binadamu linashutumu katika taarifa kwa vyombo vya habari kile inachoelezea kama "uhalifu wa kivita" na ambao unaweza pia kujumuisha "uhalifu dhidi ya binadamu". "Angalau wanawake na wasichana 66" walibakwa na "kundi lenye silaha la M23, linaloungwa mkono na Rwanda", linabainisha shirika la Amnesty International katika taarifa.

Kulingana na Amnesty International, vitendo hivi hasa vilifanyika katika wilaya ya Kishishe, yapata kilomita 100 kaskazini mwa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini wenye zaidi ya wakazi milioni moja, ambao leo umezingirwa kabisa na waasi.

Umoja wa Mataifa kwa upande wake ulisema wiki iliyopita kuwa eneo la Kishishe na viunga yvake vilikumbwa na mashambulizi mwishoni mwa mwezi Novemba ambapo takriban watu 171 waliuawa na wanawake na wasichana 27 kubakwa na waasi wa M23 kwa kulipiza kisasi mashambulizi ya makundi yenye silaha.

"Baada ya kuchukua udhibiti wa Kishishe, wapiganaji wa M23 walikwenda nyumba kwa nyumba, na kuua kila mtu mzima wa kiume waliyemkuta na kuwabaka makumi ya wanawake, ikiwa ni pamoja na visa vya mwanamke mmoja kubakwa na waasi wengi," Amnesty imesema.

Mmoja wa waathiriwa wa ubakaji ameliiambia shiriko hilo kwamba "amehesabu hadi miili 80 ya wanaume waliouawa na waasi wa M23" kanisani.

Waasi wa M23 ambao wengi wao ni Watutsi walichukua tena silaha mwishoni mwa 2021, baada ya karibu muongo mmoja kutimuliwa na kwenda uhamishoni katika nchi jirani za Rwanda na Uganda, na miongoni mwa matakwa yao makuu ni kuondolewa kwa FDLR, kundi lililoanzishwa nchini DRC na waliokuwa viongozi wa mauaji ya kimbari mwaka 1994 nchini Rwanda.

DRC inaishutumu jirani yake Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi hao, jambo ambalo linathibitishwa na wataalamu kutoka Umoja wa Mataifa, Marekani na mataifa mengine ya Magharibi, ingawa Kigali inakanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.